Home Kitaifa DC – KHERI JAMES AFUNGUA MKUTANO WA TANESCO NA WAKANDARASI.

DC – KHERI JAMES AFUNGUA MKUTANO WA TANESCO NA WAKANDARASI.

Mkuu wa wilaya ya Iringa Mhe. Kheri James mapema leo amefungua mkutano wa kimkakati baina ya TANESCO na Wakandarasi wenye leseni za umeme mkoani Iringa, wenye lengo la kujenga uelewa wa pamoja katika mikakati ya kuboresha huduma.

Akizungumza katika mkutano huo uliofanyika katika ukumbi wa Royal Palm Manispaa ya Iringa, Mhe. Kheri James ameipongeza TANESCO kwa uamuzi huo ambao utawasaidia kuwajengea uwezo wakandarasi, Utawapa nafasi ya kuwahabarisha wadau juu mageuzi ya huduma na kupokea mawazo na Ushauri utakao boresha mipango na maamuzi ya Shirika.

Aidha Mhe. Kheri James amewasihi wakandarasi wote wenye leseni kufanya kazi kwa kuzingatia weledi, usalama, ubora na gharama nafuu kwa Wananchi ili kila mwananchi awe na uwezo wa kumudu gharama.

Pamoja na mambo mengine Mhe. Kheri James ameeleza kuwa Serikali imejipanga kuhakikisha inazalisha umeme wa kutosha, na inakamilisha kwa kasi zoezi la usambazaji wa umeme katika maeneo yote ili kuimarisha huduma na uchumi wa wananchi. Akitolea mfano wa wilaya ya Iringa, Mhe. Kheri James ameeleza kuwa Serikali imekamilisha zoezi la kusambaza umeme katika vijiji vyote na sasa imetenga kiasi cha Shilingi Bilioni 26 ili kwenda kuanza hatua ya vitongoji.

Wakizungumza katika mkutano huo, Wakandarasi wameipongeza TANESCO na wameahidi kushirikiana kikamilifu ili kutekeleza kwa vitendo mambo walio Jifunza.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!