Home Kitaifa DC JOKATE, WAFANYABIASHARA, WAKULIMA MKONGE KOROGWE WAONA FURSA BANDARI YA TANGA

DC JOKATE, WAFANYABIASHARA, WAKULIMA MKONGE KOROGWE WAONA FURSA BANDARI YA TANGA

Boniface Gideon, TANGA

Mkuu wa Wilaya ya Korogwe mkoani Tanga Jokate Mwegelo ameongozo jopo la Wafanyabiashara na Wadau wa Maendeleo zikiwemo Benki mbalimbali pamoja na Watumishi wa Halmashauri mbili za Wilaya hiyo Korogwe Mji na Korogwe Vijijini kutembelea Bandari ya Tanga.

Ziara hiyo ya siku moja Bandarini hapo ilikuwa na Lengo la kuwakutanisha Wafanyabiashara,wakulima na Wamiliki wa Viwanda vya kuchakata zao la Mkonge Kutumia Bandari hiyo katika Usafirishaji wa mizigo kwenda nje ya Nchi.

Katika ziara hiyo Wakulima zaidi ya 2000 wa zao la Mkonge waliopo katika vikundi vya Amcos wilaya ya Korogwe Mkoani Tanga walipata fursa yakueleza changamoto wanazokabiliwa nazo ikiwamo ukosefu wa mashine bora kwaajili ya kuchakata zao hilo mara baada ya kutoka shambani hali inayopelekea kupata hasara na kuchakata kiwango cha chini ya kiwango licha ya wananchi wengi kuhamasika kujihusisha na kilimo hicho.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!