Home Kitaifa DC HAULE AWATANGAZIA KIAMA WEZI WA MIUNDOMBINU YA MAJI MUSOMA VIJIJINI

DC HAULE AWATANGAZIA KIAMA WEZI WA MIUNDOMBINU YA MAJI MUSOMA VIJIJINI

-WATAKAOKAMATWA KUFUNGULIWA KESI YA UHUJUMU UCHUMI

Na Shomari Binda-Musoma

MWENYEKITI wa Kamati ya Ulinzi na Usalama Wilaya ya Musoma na mkuu wa Wilaya hiyo Dk.Khalfan Haule ametangaza kuchukuliwa hatua kali za kisheria watakaobainika na kukamatwa wezi wa miundombinu ya maji.

Akuzungumza na Mzawa Blog ofisini kwake amesema kamwe hawatavumiliwa wanaofanya hujuma hizo na kuwakosesha wananchi huduma muhimu ya maji.

Amesema watu hao wamekuwa wskiiba miundombinu hiyo na kwenda kuweka kwenye vyoo majumbani mwao kwa masrahi binafsi.

Dc Haule amesema wananchi wanapaswa kuwa walinzi wa kwanza wa miundombinu hiyo ya maji kwa kuwa wezi hao wanaishi nao.

Amesema huo ni uhujumu uchumi na yeyote atakayekamatwa akiiba miundombinu ya maji atafunguliwa kesi ya uhujumu uchumi.

Tumefanya kikao cha wadau wa maji yapo mambo ya msingi tumeyazungumzia kuhusiana na huduma ya maji kwa wananchi wetu.

Lipo jambo baya limeibuka la wizi wa miundombinu ya maji tutamshughulikia kila mmoja anayefanya tabia hii na wananchi wawe walinzi wa kwanza kwenye jambo hili“,amesema Haule.

Wakati huo huo vijiji vyote 68 vya jimbo la Musoma Vijijini vinasambaziwa maji safi na salama ya bomba kutoka Ziwa Victoria.

Miradi hiyo ya usambazaji maji ya bomba iko kwenye hatua mbalimbali za utekelezaji. Usambazi maji ya bomba vijijini unafanywa na RUWASA, MUWASA na mradi wa Mugango-Kiabakari-Butiama

Mbunge wa jimbo la Mudoma vijijiji pamoja na wananchi wameendelea kutoa shukrani kwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kutoa fedha nyingi kwaajili ya miradi ya maji.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!