Home Kitaifa DC HAULE AWATAKA WANANCHI KUCHANGAMKIA ZOEZI LA UPIMAJI ARDHI NA KUPATA HATI

DC HAULE AWATAKA WANANCHI KUCHANGAMKIA ZOEZI LA UPIMAJI ARDHI NA KUPATA HATI

Na Shomari Binda-Musoma

MKUU wa Wilaya ya Musoma Dkt. Khalfan Haule amewataka wananchi kuchangamkia zoezi la upimaji wa ardhi na kupata hati za umiliki.

Kauli hiyo ameitoa Kata ya Nyakato manispaa ya Musoma alipokuwa akigawa hati kwa wananchi 70 ambao walikuwa wamepimiwa viwanja vyao.

Amesema zoezi la upimaji viwanja linaendeshwa na maafisa ardhi wa manispaa ya Musoma na mkoa wa Mara na kuwaomba wananchi kuchangamkia fursa hiyo.

DC Haule amesema hati kuwa nayo ina umuhimu mkubwa katika umiliki wa ardhi ambayo uwezesha hata kupata mikopo kutoka taasisi za kifedha.

Amesema unapokuwa na hati na unataka kuongeza mtaji kwenye biashara unaweza kufika kwenye taasisi za kifedha ukaongezewa mtaji.

Mkuu huyo wa wilaya amesema wananchi wenye maeneo ya viwanja ambavyo havijapimwa wanaweza kufika ofisi za ardhi wakapewa utaratibu na kupimiwa viwanja vyao.

“Nichukue fursa hii kuwapongeza wananchi ambao leo mnapokea hati zenu za umiliki wa ardhi ambazo zitawaaidia kwenye masuala mbalimbali”

“Kwa wale wenye viwanja ambavyo havijapimwa ni vyema wakafika ofisi za ardhi wakapata utaratibu wa kupimiwa na hati hutolewa kwa muda mfupi”, amesema DC Haule.

Kwa upande wao wananchi waliopokea hati hizo wameishukiru serikali kwa kutoa hati kwa muda mfupi tofauti na zamani.

Wemesema kipindi cha nyuma hati ilikulazimu kusafiri hadi Mwanza kufuata hati na sasa wanazipata wakiwa Musoma.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!