Home Kitaifa DC HAULE AENDELEA KUPOKEA KERO ZA WANANCHI KUHUSU MIGOGORO YA ARDHI MANISPAA...

DC HAULE AENDELEA KUPOKEA KERO ZA WANANCHI KUHUSU MIGOGORO YA ARDHI MANISPAA YA MUSOMA

Na Shomari Binda-Musoma

MKUU wa wilaya ya Musoma Dkt. Khalfan Haule ameendelea kupokea kero za wananchi kuhusiana na migogoro ya ardhi manispaa ya Musoma.

Kero na migogoro ya ardhi inaendelea kupokelewa kwa siku 5 kwenye kliniki ya migogoro kwa mkoa wa Mara iliyozinduliwa novemba 21 na mkuu wa mkoa wa Mara Said Mtanda kwenye uwanja wa shule ya msingi Mukendo.

Katika siku ya pili mkuu huyo wa wilaya amepokea kero na migogoro 30 na kuifanyia kazi na mingine kutoa maelekezo kwa maafisa ardhi wa halmashauri ya manispaa ya Musoma kufika maeneo ya migogoro na kuipatia ufumbuzi na kupata taarifa.

Akizungumza na Mzawa Blog mkuu wa wilaya ya Musoma Dkt. Haule amesema amekaa kwa siku nzima kwenye uwanja wa shule ya msingi Mukendo na migogoro mingi aliyoisikiliza inahusiana na maeneo ya mipaka.

Amesema baada ya kusikiliza migogoro hiyo ipo iliyofanyiwa kazi papo hapo na mingine imetolewa maelekezo kwa maafisa ardhi kufika eneo la migogoro na kuitolea taarifa utatuzi wake.

“Tumeendelea kupokea na kusikiliza kero za wananchi zinazohusiana na migogoro ya ardhi na kuipatia ufumbuzi”

“Haya ni maelekezo na maagizo ya mkuu wa mkoa wakati wa uzinduzi wa kliniki ya kusikiliza migogoro ya ardhi na tumeendelea kuwasikiliza wananchi” amesema DC Haule.

Amesema kwa siku 3 zilizobaki wananchi wanapaswa kufika kwenye uwanja wa shule ya msingi Mukendo na kutoa kero zao za migogoro ya ardhi ili iweze kusikilizwa.

Amesema wananchi wasisubili ujio wa viongozi wa kitaifa na kusimama na mabango bali watumie fursa hiyo kufika kwenye kliniki ya utatuzi ili wasikilizwe.

Wananchi wa manispaa ya Musoma wameendelea kujitokeza na kutoa kero zao na kumshukuru ofisi ya mkuu wa mkoa kwa kuiandaa.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!