Home Kitaifa DC CHIKOKA AWATAKA WANANCHI WALIOPATA MIKOPO YA ASILIMIA 10 YA MAMA SAMIA...

DC CHIKOKA AWATAKA WANANCHI WALIOPATA MIKOPO YA ASILIMIA 10 YA MAMA SAMIA KUITUMIA KWA MALENGO

Na Shomari Binda-Musoma

MKUU wa Wilaya ya Musoma Juma Chikoka amewataka wananchi kuitumia kwa malengo mikopo ya asilimia 10 waliyoipata kutoka halmashauri ya Musoma vijijini.

Vikundi 21 vya halmashauri hiyo vimepewa mikopo kiasi cha milioni 400 baada ya dilisha kufunguliwa rasmi baada ya kusitishwa kwa muda.

Akizungumza baada ya zoezi la kukabidhiwa hundi za fedha hizo lililofanyika kwenye ukumbi wa halmashauri ya Musoma Chikoka amesema fedha hizo zitumike kuinua uchumi.

Amesema lengo la serikali ya Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan ni kuona wananchi wanainuka kiuchumi na kutoa mikopo isiyokuwa na riba.

Chikoka amesema mikopo hiyo ni mwanzo na vikundi vingine zaidi vitaendelea kuwezeshwa na kuvitaka vikundi vilivyopata kurejesha muda ukifika.

‘” Pochi la Mama limefunguka twende tukaitumie mikopo hii kwa lengo lililokusudiwa ili kujiinua kiuchumi”,amesema.

Mbunge wa jimbo la Musoma vijijini Profesa Sospeter Muhongo aliyehudhuria tukio hilo amesema ni vyema mikopo hiyo ikatumika kwenye uzalishaji kwani kuna manufaa zaidi.

Amesema maeneo ya kilimo na uvuvi yana fursa kubwa na kuwataka wananchi kuyaona maeneo hayo kuyatumia.

Baadhi ya wananchi waliopata mikopo hiyo wameishukuru serikali kwa kuwawezesha mikopo hiyo na kuahidi kuitumia kujiinua kiuchumi na kuirejesha.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!