Na Shomari Binda-Musoma
MKUU wa Wilaya ya Rorya Juma Chikoka ambaye pia ni Kaimu Mkuu wa Wilaya ya Musoma amewapongeza madiwani wa manispaa ya Musoma kwa kasi ya kuwaletea wananchi maendeleo.
Licha ya pongezi hizo ametoa ushauri kwa madiwani kuwa wabunifu kwenye vyanzo vipya vya mapato ili kukuza ukusanyaji wa mspato ya ndani.
Pongezi na ushauri huo ameutoa kwenye kikao cha baraza la madiwani alipokuwa akitoa salamu za serikali.
Amesema manispaa ni kioo cha hslmashauri nyingine katika kujifunza hivyo ni muhimu kuwa na vitu vya mfano ili wengine kujifunza.
Chikoka amesema amefika kwa mara ya kwanza na kuona vitu vya tofauti ikiwa ni pamoja na madiwani kutoa michango inayolenga kuwaletea wananchi maendeleo
“Leo nimepata bahati ya kuhudhuria kikao hiki cha baraza la madiwani lakini nikili nimejifunza mengi kutoka kwenu kutokana na michango mnayochangia”
“Mnayo dhamira ya kuwaletea maendeleo wananchi na hilo ndio lengo la serikali ya awamu ya 6 ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan” ,amesema Chikoka.
Amesema ili kuongeza mapato ya halmashauri na wengine kujifunza upo umuhimu wa kubuni vyanzo vipya vya mapato ndani ya manispaa ya Musoma.
Katika hatua nyingine DC Chikoka amesema serikali imekuwa ikitoa fedha nyingi kwaajili ya miradi mbalimbali na kuwaomba madiwani kuwa wafatiliaji na wasimamizi ili iweze kuwanufaisha wananchi.
Katika michango yao ya taarifa mbalimbali za kamati madiwani hao wamesema ushauri wa Kaimu mkuu huyo WS Wilaya ni wa kuzingatiwa ikiwa ni pamoja na kutazama upya ikiwa ni pamoja na makusanyo ya vyombo vya moto
Akihairisha baraza hilo la robo ya kwanza Meya wa manispaa ya Musoma Patrick Gumbo amesema mapato ndio msingi wa kusimama na kuimalika kwa manispaa na kuwaomba madiwani kupokea ushauri uliotolewa wa kuongeza vyanzo na ufatiliaji wa makusanyo wa vyanzo vilivyopo.