Home Kitaifa DC BUKOBA APONGEZA UJIO WA GAZETI LA MONTESSORI TANZANIA ASEMA LITAKUWA MSAADA...

DC BUKOBA APONGEZA UJIO WA GAZETI LA MONTESSORI TANZANIA ASEMA LITAKUWA MSAADA MKUBWA KATIKA JAMII

Na Theophilida Felician Kagera.

Mkuu wa wilaya Bukoba Mhe Erasto Sima apongeza ujio wa gazeti la MONTESSORI TANZANIA Mkoani Kagera chini ya Mkurugenzi wake Bi Jacqueline Mwombeki.

Mkuu wa wilaya Sima ameyasema hayo akiwa Mgeni rasmi kwaniaba ya Mkuu wa Mkoa Kagera Mhe Fatma Mwassa katika hafla ya uzinduzi wa gazati hilo Manispaa ya Bukoba.

Baada ya kupata melezeo ya adhima ya kuanzishwa kwa gazeti hilo kutoka kwa Mkurugenzi wake ameelezea kuvutiwa na maelezo hayo ambayo yamejikita zaidi kuzungumzia masuala mazima ya kutoa elimu kwa makundi tofauti tofauti hususani katika malezi bora na elimu kwa watoto.

“Kwakweli kama taarifa ilivyosomwa hapa wote tumeelewa vizuri gazeti hili litakuwa ni msaada mkubwa, mimi niwapongeze sana MONTESSORI FOR ALL mambo yake nchi nzima tunaona yanavyoendelea imekuwa na malezi mazuri hasa kwa watoto wadogo sisi ambao tumekuwa tukifika maeneo mbalimbali ya nchi tumekuwa tukishuhudia kazi zake sasa wamekuja na gazeti tunaimani kwa jinsi mlivyo kwenye malezi ya watoto hivyo hivyo na mambo ya gazati yatakuwa mazuri nayenye tija” amesema Erasto Sima Mkuu wa wilaya.

Amefafanua kwamba kulingana namaono yao ya kuisemea jamii ya Kagera na Taifa itayaibua mambo mengi ya changamoto za wananchi kwa malengo ya kufanyiwa utatuzi ambapo ametole mfano wa changamoto yakutokutolewa kwa usahihi taarifa za matukio ya ukatili na unyanyasaji kijinsia ambayo yamekuwa yakijitokeza kwa jamii na mwisho kuyaficha hivyo kupitia gazati hilo litakuwa jicho lakipekee katika kuyaibua nakuyasema.

Pia amesema litayatangaza mengi ya mafanikio ya maendeleo yanayotekelezwa na Serikali Mkoani Kagera na kwingineko kwa maana kwamba mpaka sasa fedha nyingi zimekuwa zikiletwa Kagera kwa ajili ya ujenzi wa miradi ya maendeleo ya wananchi.

“Mafanikio mengi ya Serikali yetu yapaswa kusemwa hata kituo chetu cha mabasi walisema hakijengwi sasa kitajengwa nakama kuna kitu kinamkosesha usingizi Mkuu wetu wa mkoa pamoja na sisi ni hicho kituo chetu mvua zikianza hapa tunajua mziki watope lile sasa tunaenda kulikamilisha hilo jambo kiwepo kituo cha kisasa na wazo la kituo kile cha Kyakaibwa linaendelea lakini kwa sasa tukijenge kile kikamilike ili tuweze kuondokana na adha ile ya tope” amesisitiza Mkuu wa wilaya huo.

Amewaomba MOTESSORI FOR ALL kuendelea kubuni mambo mengine kama walivyo buni kuanzisha kwa gazeti kwani serikali iko nao bega kwa bega katika kuwapa ushirikiano huku akiwasihi wana Kagera wakiwemo wadau tofauti tofauti kulitumia kwa mambo kadha wa kadha kwa malengo ya kujenga.

Jacqueline Mwombeki Mkurugenzi wa gazeti hilo ameeleza kuwa gazeti hilo litakaloanza rasmi shughulizake Tarahe 2 October mwaka huu wa 2023 limebebwa na kauli mbiu ya ELIMU NA MALEZI, zaidi linajikita kuandika makala endelevu zinazolenga kumshirikisha mzazi, mlezi na jamii kwa ujumla namna njema ya kulea, kuonya na kukanya ili kupunguza tatizo la mienendo inayopelekea mmomonyoko wa maadili katika jamii lakini pia umuhimu wa matumizi ya lugha rafiki katika ufanisi wa shughuli yoyote ile, kutambua fursa za uchumi, mbinu na uboleshaji wa elimu shuleni, sambamba na kukumbushana wajibu wa ustawi.

Aidha amesema ni matarajio yao kuwa miaka 12 ijayo kupitia makala za MONTESSORI TANZANIA kwa Tanzania litakuwa nilakuigwa na kuwa na jamii fanisi kwa nyanja za elimu na malezi vilivyo bora zaidi.

Amehimiza kuwa gazeti hilo nila watu wote hivyo wasisite kulitumia kwa ukarbu.

Kemilembe Ndyamukama akisoma risala amebainisha kuwa gazati hilo linalozalishwa Mkoani Kagera limesajiliwa kwa mjibu wa sheria linalenga kuhabarisha taifa juu ya elimu na malezi ili kumuandaa mtanzania mwenye maadili na tamaduni zinazokubalika kitaifa.

Ameongeza nakusema kuwa litawaunganisha nakuleta majibu ya maswali yaliyopo kwenye jamii kupitia makala zenye elimu mbalimbali zinazolenga kumuandaa mtanzania mwenye uzalendo wakweli mwajibikaji, mbunifu, na mwenyekujitegemea katika kutambua wajibu na nafasi yake kwa taifa.

Risala hiyo imesisitiza kuwa gazeti hilo kwakushirikiana kikamilifu na Serikali, wadau wamaendeleo na jamii kupitia elimu nambinu shirikishi elimu kwa vitendo na lugha rafiki vitamfanya kila mmoja kutimiza wajibu wake katika malezi na elimu maana mtu anakamilika nakuwa mwenye tija anapokuwa ameyapata kikamilifu mambo hayo mawili.

Hata hivyo gazeti hilo litajikita kuitambua michango ya wadau wa maendeleo, shughuli za maendeleo zinazofanywa na Serikali na watanzania wote kwani ndani yake kuna vipengere husika na mambo hayo ambavyo ni Historia yangu na Hapa nilipo.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!