Home Kitaifa DC AWAUNGA MKONO WANANCHI BAADA YA KUCHANGISHANA MILIONI 6.5 KUJENGA MRADI WAO...

DC AWAUNGA MKONO WANANCHI BAADA YA KUCHANGISHANA MILIONI 6.5 KUJENGA MRADI WAO WA MAJI

Wananchi wa kijiji cha Lusitu kata ya Luponde Halmashauri ya mji wa Njombe wamelazimika kuchangishana zaidi ya shilingi milioni 6.5 ili kujenga mradi wa maji utakaowasaidia kuepukana na adha ya kufuata maji mabondeni hadi majira ya usiku.

Hatua hiyo imekuja kufuatia kukosa maji ya bomba ilihali vijiji vingine vya kata ya Luponde vikiwa na maji jambo lililowasukuma kuchukua jitihada binafsi badala ya kuendelea kuisubiri serikali iwasaidie.

Kutokana na Jitihada za wakazi hao Serikali ya wilaya ya Njombe chini ya Mkuu wake wa Wilaya Kissa Gwakisa Kasongwa na kamati yake ya Ulinzi na Usalama imelazimika kufika na kuwaunga mkono kwa kuchangia zaidi ya milioni moja huku akiagiza Wakala wa Maji vijijini Ruwasa kuhakikisha wanasaidia kupatikana maji ndani ya wiki tatu.

Mtaalamu wa Maji toka RUWASA Wilaya ya Njombe Bakari Kitogota amekiri kupokea maelekezo ya serikali na kuahidi kutoa fedha za kukamilisha mradi huo.

Baadhi ya wananchi wa Lusitu akiwemo Produse Kilumile na Salima Msigwa wameonesha furaha yao baada ya serikali ya wilaya kufika na kuwachangia fedha za kukamilisha mradi huo na kwamba sasa adha kwa akina mama zitapungua Endapo mradi utakamilika.

Kwa upande wake Mbunge wa Jimbo la Njombe Mjini Deo Mwanyika aliyechangia shilingi Milioni moja katika ujenzi wa mradi huo kupitia katibu wake Andreas Mahali ametuma ujumbe wa kulinda mradi huo utakapokamilika.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!