Home Michezo DAR BINGWA CRDB TAIFA CUP, DODOMA, UNGUJA, TANGA ZANG’ARA

DAR BINGWA CRDB TAIFA CUP, DODOMA, UNGUJA, TANGA ZANG’ARA

Na Boniface Gideon, TANGA

Michuano ya Mchezo wa Basketball Nchini Maarufu kama CRDB TAIFA CUP imemalizika mwishoni mwa Wiki usiku wa kuamkia Jana jumapili huku Mikoa ya Dar es Salaam iking’ara kwa kuchukua vikombe vyote kwa Wanaume na Wanawake huku michuano hiyo ikichukua Sura mpya Baada ya Vijana waliochini ya Miaka 21 wakionekana kung’ara zaidi.

Mkoa wa Dar es Salaam imeibuka Bingwa wa Jumla Baada ya Timu zote mbili za Wanaume na Wanawake kutwaa Ubingwa huku kila Timu ikijinyakulia Sh.10Mil kama zawadi kutoka kwa Wadhamini wa Michuano hiyo Benki ya CRDB .

Mkoa wa Dodoma nao umetwaa nafasi ya pili kwa Wanawake na Wanaume hivyo kufanya zawadi za Kubwa kwenda katika Mikoa hiyo miwili, Mikoa ya Tanga na Unguja imemaliza kwenye nafasi nne(4) za juu , Timu zilizoshiriki michuano hiyo ni 36 Wanaume Timu 20 na Timu za Wanawake 16 Tanzania Bara na Visiwani .

Akifunga Mashindano hayo Waziri wa Michezo,Sanaa na Utamaduni Mohamed Mchengerwa aliwapongeza Wanamichezo pamoja Waandaji wa Mashindano hayo kwakuandaa kwa viwango vya Hali ya juu Hali iliyofanya michuano hiyo kuwa na msisimko mkubwa kwa Mashabiki wa Wananchi mkoani Tanga na Nchi nzima kwa Ujumla.

Waziri Mchengerwa Alisema Serikali imeweka Mazingira rafiki ya Ujenzi wa Miundombinu ya Michezo Nchini ikiwamo Ujenzi wa Viwanja vya kisasa nakwa kwa yeyote anayehitaji Kujenga Viwanja vya Michezo Serikali itampa Ushirikiano na Vibali kwa Wakati,

“Kupitia hili Niwaombe Wakuu wa Mikoa, Wakuu wa Wilaya,Wakurugenzi wa Halmashauri pamoja na Madiwani wajitahidi angalau tuwe na Bajeti ya Kujenga Viwanja vya Michezo, Uwanja wa Basketball hauna gharama kubwa sana hivyo Halmashauri inaweza ikatenga Bajeti yake na ikafanikisha Ujenzi kwa urahisi, na sisi Wizara tutoa Ushirikiano” Alisisitiza

Kauli Ujenzi wa Viwanja ya Waziri Mchengerwa ilikuwa akisisitiza kauli ya Mkuu wa Mkoa wa Tanga Omar Mgumba ambaye Awali Alisema Mkoa wa Tanga umetenga eneo maalumu la ekari 300 kwaajili ya Ujenzi wa Viwanja vya Michezo Wilayani Mkinga,

Sisi Mkoa wa Tanga hatuna Dogo ili kuhakikisha mashindano haya yanafanyika mkoani Tanga, Mkoa wa Tanga umetenga eneo maalumu la Ekari 300 kwaajili ya Ujenzi wa Viwanja vya Michezo mbalimbali ili kutoa Fursa kwa Vijana Wengi kuingia kwenye Sekta hii ya Michezo lakini, tunataka Mkoa wa Tanga Uwe kitovu Cha Michezo Nchini na kwakufanya hivyo ni lazima tuwe na Viwanja na Ndio Mana tumetenga Ekari 300 kwaajili ya Ujenzi wa Viwanja mbalimbali ” Alisisitiza Mgumba

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!