Home Burudani DAIMOND PLATINUM NA WADAU WENGINE WAGUSWA KUMSAIDIA JACKLINE MTAITA

DAIMOND PLATINUM NA WADAU WENGINE WAGUSWA KUMSAIDIA JACKLINE MTAITA

Na. Magrethy Katengu, Mzawa

Jackline Bakari(23) ambaye ni mlemavu wa miguu na ni muimbaji wa nyimbo za bongo fleva ameamua kujitoleza hadharani kuomba msaada Kwa kusaidiwa kuinua kipaji chake ili aweze kujikwamua kiuchumi ikiwemo kujiendeleza kimasomo

Akizungumza na waandishi Habari jijini Dar es salaam Jackline Bakari amesema kuwa hali hiyo ulemavu ilimpata kwenye ajali January 4 ,2020 wakati akienda shuleni mkoani kagera kutokana na kuugua alikatisha masomo yake hivyo akaanza kutunga nyimbo mbalimbali akiamini kuwa siku Moja ndoto yake itatimia japo itachelewa.

Ninaomba Mama Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamuhuri wa Muunganao wa Tanzania aweze kunisaidia tena iliniweze kusimama tena kwani naamini ninaweza bado sijakata tamaa Mungu yupo upande wangu kama aliniokoa kupona katika ajali ile anaweza kunipatia kila hitaji ninalomuomba “amesema Jackline.

Naye Mwenyekiti wa Taasisi ya MAMA ONGE NA MWANAO ambaye pia Msaani wa Maigizo Steveen Nyerere wakati akiongea na simi na Muimbaji Maarufu wa nyimbo za Muziki wa kibongo Abduli Nasibu kwa jina Maarufu Diamond Platinum aliahidi kumsaidia kurekodi nyimbo zake katika Lebo ya WCB na nyimbo zake kurushwa katika Tv na Redio ya Wasfi pia kufanyiwa mahojiano maalumu ili aweze kujulikana

Jackline anakwenda kuinuka kimziki katika lebo ya Mziki WCB masaada alioupata na wadau mbalimbali wanaendelea kujitoleza kumsaidia ilikuendeleza kupaji cha chake nimsihi sana asikate tamaa
hali ya ulemavu ni hali ya kawaida hivyo kila Mwanadamu anachangamoto yake akupitia hivyo alivyo anaweza kufanya Mambo makubwa “amesema Steven

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!