WAWEZA KUTAZAMA VIDEO HAPA
Na Mwandishi Wetu.
Saada Omary Mfanyabiashara ya Upishi, Mkazi wa Ilala Jijini Dar Es Salaam ni miongoni mwa washindi wa Milioni Moja, Kampeni ya Tigo CHA WOTE wiki ya Nne ambapo hadi sasa Tigo wameshatoa Fedha Taslim na zawadi mbalimbali kwa Washindi Takribani 9000 ( Elf u Tisa) Nchi Nzima tangu kampeni hii izinduliwe.
Akizungumza Leo Julai 21, 2023. Wakati wa Kuwakabidhi Mfano wa Hundi Baadhi ya Washindi wa Milioni Moja Moja wiki ya nne waliobahatika kufika Tigo Makao Makuu, Meneja Wa Wateja Maalum Tigo Pesa Bi Mary Rutha amesema kuwa hadi sasa ikiwa ni wiki Nne tu tangu Kampeni iyo izinduliwe wameshapatikana washindi Takribani 9000 kutoka maeneo mbalimbali nchini .
” Leo tunayo furaha kubwa kuwa na baadhi ya washindi wa Wiki ya Nne wa Kampeni ya TIGO CHA WOTE ambao hawa ni washindi wa Milioni Moja Moja kila mmoja, Lakini niwakumbushe Watanzania kwamba kila siku CHA WOTE inatoa zawadi ikiwemo pesa taslimu hadi Milioni Moja kwa washindi 320 kila siku , kuibuka mshindi ni rahisi tu unachotakiwa ni kufanya miamala na Tigo Pesa kama Kutumia Lipa Kwa Simu , Kununua Vifurushi , Kulipia Bili kwa Tigo Pesa , n.k kwa kufanya ivyo nawewe siku si nyingi utakua miongoni mwa Washindi wa Kampeni hii ya CHA WOTE “. ” Alisema Bi. Mary Rutha
Naye Mmoja wa Washindi wa Milioni Moja, Saada Omary mfanyabiashara ya Upishi kutoka Ilala Dar Es Salaam amesema kuwa ana furaha kubwa kuibuka mshindi wa Kampeni hii na hakutegemea kama hata Watanzania wenye kipato cha kawaida wanaweza kushinda
” Kwakweli nikiri nimefurahi sana jamani , Mimi Nafanya biashara ya Kupika na huwa nafanya miamala mbalimbali kama kulipia bili , na kununua Vifurushi vya SMS na Muda wa Maongezi nafikiri ivyo ndo vimenifanya nkawa mshindi , kwakweli hakika hiii ni CHA WOTE maana kumbe inawezekana kila mtu akawa mshindi hata sisi wenye kipato cha kawaida , katika maisha yangu Sikumbuki kama nilishawahi kushinda chochote, hii milioni moja inaenda kubadilisha Biashara Yangu kwa maana kuna Vyombo nlikua natamani kuwa navyo na sasa naenda kuvinunua ili nirahisishe Biashara Yangu ” Alisema Bi. Saada Muda mchache baada ya Kukabidhiwa Hundi yake ya Milioni Moja Makao Makuu ya Tigo Kijitonyama Jijini Dar es Salaam.
Mshindi Mwingine aliyebahati kukabidhiwa Hundi yake Leo hii Tigo Makao Makuu ni Bi. Tausi Makoba Mkazi wa Makongo Dar Es Salaam.