Katika kuendeleza jitihada zake za kuwajengea uwezo na kuwawezesha wajasiriamali vijana nchini, Benki ya CRDB leo iliandaa semina maalum iliyopewa jina la “CRDB Bank Instaprenyua”, iliyofanyika 16 Julai 2022 katika Makao Makuu ya Benki hiyo, kwa ajili ya kuwawezesha vijana ambao wanafanyabishara kupitia mitandao ya kijamii.
Akizungumza wakati akifungua semina hiyo, Afisa Mkuu wa Biashara wa Benki ya CRDB, Boma Raballa alisema katika miaka ya hivi karibuni kumekuwa na mwamko mkubwa kwa vijana kujishughulisha na shughuli za ujasiriamali hususani kupitia mitandao ya kijamii ambayo imerahisisha namna ya kuendesha biashara, na kuyafikia masoko kwa urahisi.
“Vijana wamekuwa wakitumia vizuri fursa zilizopo hususani fursa za mitandao ya kijamii kufanikisha shughuli zao za ujasiriamali. Tumewaona vijana wajasiriamali ambao wanafanya vizuri kupitia maduka mtandao, jambo ambalo limetusukuma kuwapa elimu na kuwajengea uwezo,” alisema Raballa.
Aliendelea kusema biashara mtandao ni moja ya eneo linalokua kwa kasi, na linalopaswa kuangaliwa, ikiwa ni pamoja na kutafuta suluhu ya kuwawezesha wajasiriamali hao. Mitandao ya kijamii hususan Instagram, Facebook na Twitter imekuwa chachu kubwa kwa vijana wajasiriamali hapa nchini kuishi ndoto zao za ujasiriamali.
Takwimu zinaonyesha Instagram ndio mtandao wa kijamii wenye watumiaaji wengi zaidi duniani, bilioni 1.074, vivyo hivyo hapa Tanzania, mtandao huo unaongoza pia kwa wafuasi zaidi ya milioni 2.86. “Hii ndio sababu ya kuipa jina la Instaprenyua semina hii kwani ndipo hasa vijana wengi wapo, lakini lengo ni kuwafikia vijana katika majukwaa yote ya mtandaoni,” aliongezea.
Akizungumzia kuhusu malengo ya kuandaa semina hiyo, Mkuu wa Kitengo cha Masoko wa Benki ya CRDB, Joseline Kamuhanda, alisema Semina hiyo ina malengo makuu matano ikiwamo; kutoa mafunzo ya namna bora ya kuendesha biashara kwa wajasiliamali wanaofanya biashara mtandao, na kutoa elimu ya usimamizi wa fedha katika biashara.
Malengo mengine ni pamoja na elimu ya masoko ya fedha na mitaji, na namna bora za kuyaendea masoko hayo, elimu juu ya fursa zinazotolewa na Benki ya CRDB kwa wajasiriamali nchini, pamoja na elimu ya urasimishaji wa biashara, na faida zake kwa wajasiriamali.
Afisa Mkuu wa Biashara wa Benki ya CRDB, Boma Raballa akizungumza wakati wa semina maalum kwa ajili ya kuwawezesha vijana ambao wanafanyabishara kupitia mitandao ya kijamii iliyopewa jina la “CRDB Bank Instaprenyua”, iliyofanyika, Julai 16 2022 katika Makao Makuu ya Benki ya CRDB yaliyopo Barabara ya Ali Hassan Mwinyi, jijini Dar es salaam. Wengine pichani kutoka kulia ni Mkuu wa Kitengo cha Masoko wa Benki ya CRDB, Joseline Kamuhanda, Mkurugenzi wa Swahili Digital, Gillsant Mlaseko pamoja na Mkuu wa Kitengo cha Huduma kwa Wateja wa Benki ya CRDB, Yolanda Urio.
Mkuu wa Kitengo cha Huduma kwa Wateja wa Benki ya CRDB, Yolanda Urioakizungumza wakati akiwasilisha mada yake katika semina maalum kwa ajili ya kuwawezesha vijana ambao wanafanyabishara kupitia mitandao ya kijamii iliyopewa jina la “CRDB Bank Instaprenyua”, iliyofanyika, Julai 16 2022 katika Makao Makuu ya Benki ya CRDB yaliyopo Barabara ya Ali Hassan Mwinyi, jijini Dar es salaam.
Mkuu wa Kitengo cha Masoko wa Benki ya CRDB, Joseline Kamuhanda akizungumzia umuhimu wa kumthamini mteja katika biashara, wakati wa semina maalum kwa ajili ya kuwawezesha vijana ambao wanafanyabishara kupitia mitandao ya kijamii iliyopewa jina la “CRDB Bank Instaprenyua”, iliyofanyika, Julai 16 2022 katika Makao Makuu ya Benki ya CRDB yaliyopo Barabara ya Ali Hassan Mwinyi, jijini Dar es salaam.
Mkurugenzi wa Swahili Digital, Gillsant Mlaseko ambaye alikuwa ni mmoja wa watoa mada katika semina maalum kwa ajili ya kuwawezesha vijana ambao wanafanyabishara kupitia mitandao ya kijamii akizungumza , katika semina hiyo iliyopewa jina la “CRDB Bank Instaprenyua”, iliyofanyika, Julai 16 2022 katika Makao Makuu ya Benki ya CRDB yaliyopo Barabara ya Ali Hassan Mwinyi, jijini Dar es salaam.