Home Kitaifa CHUO KIKUU SUZA CHAJA NA FUSRA MPYA YA KOZI IKIWEMO SHAHADA YA...

CHUO KIKUU SUZA CHAJA NA FUSRA MPYA YA KOZI IKIWEMO SHAHADA YA AWALI YA SAYANSI YA MAABARA

Na Magrethy Katengu

Chuo Kikuu Cha Taifa, Zanzibar (SUZA) kimekuja na fursa mpya programme {kozi} mbili ikiwemo ya shahada ya awali ya sayansi ya maabara pamoja na shahada uzamili ya uendeshaji wa biashara na fedha ikiwa ni jitihada za chuo hicho kuhakikisha wanatoa elimu bora

Akizungumza leo Jijini Dar es salaam na waandishi wa habari Mkuu wa Kitengo cha Mahusiano na Masoko wa chuo hiko Khadija Mahumba katika banda lao chuo ambapo kimeshiriki K Maonesho ya 18 ya elimu ya juu sayansi na teknolojia yanayofanyika katika viwanja vya mnazi mmoja kuanzia Julai 17 hadi 22,2023 ambapo amesema chuo kina Shahada Ya Ujasiriamali Na Ubunifu ambayo Imekuwa msaada mkubwa kwa Wahitimu wa kozi hiyo kwa kanzisha biashara na kujiajiri na si kuajiriwa pekee.

Khadija amewashauri wazazi na walezi watembelee banda lao kuona fursa zilizopo katika chuo hicho ikiwemo fursa ya wataalamu wabobevu wa lugha ya kiswahili ambapo chuo hicho kimezalisha wataalu wengi wengine wamechukuliwa kwenda kufundisha nje ya nchi na bado kinaendelea kupika wanafunzi wenye ujuzi na weledi mkubwa watakaokidhi kiwango cha kimataifa.

“Chuo Chetu kimejikita kutoa kozi mbalimbali na fani Nyingi tofauti, kwani tuna fani za Afya ya,utalii, kilimo, ujasiriaamali, biashara, teknolojia ya habari (IT),Tehama lakini pia tuna fani ya sayansi ya kompyuta cha kufanya tu waje watembelee kwenye banda letu wajionee” amesema Khadija

kuhusu masomo ya kiswahili Bi Khadija amesema chuo hicho kinaendelea kutoa elimu ya shahada ya uzamili ya kiswahili kwa watumiaji wa lugha nyingine ikiwemo kichina ambapo huwaandaa wanafunzi kwa ajili ya kuwa walimu wa kiswahili kwa watumiaji wa lugha nyingine na chuo hicho pia kimebobea katika ufundishaji wa kiswahili kwa wageni kwani kina wataalam wa masomo hayo wa kutosha

Kwa upande wake mkuu wa idara ya ujasiriamali Dkt Mohamed Salum Mohamed amesema kuwa kwa mwaka huu kwa mara ya kwanza kinatoa wahitimu wa digrii ya ujasiriamali ambao watahitimu hivi karibuni ambapo ameongeza kuwa walivyoanza masomo yao waliyachukua mawazo ya kibiashara ya wanafunzi hao na kuyachakata kisha kutumia mimea na majani mbalimbali kutengeneza bidhaa.

“huwa tunawaweka wanafunzi wetu katika makundi kuanzia watu watano wenye mawazo mamoja na wanaunda kampuni na wanafanya shughuli zao ujasriamali baadaye huzisajili ili kwenda sokoni kama hii bidhaa mnayoiona hapa hawa wameamua kuitumia mimea iwe ni kama chachu ya kuwaamsha wananchi kuwa kwenye mimea kuna fursa kwani wametoa mafuta,masala,lipstic,vipodozi na wanaendelea na hatua ya kuzisajili bidhaa hizo kwenda sokoni kuuza.

Aidha amesema katika fani hiyo waliojitokeza kupenda kozi hiyo ambao wanahitimu mwaka huu wanawake ni wengi na wanaume ni wawili hii inaonyesha jinsi wanawake walivyoomyesha kipaumbele cha kuchangamkia fursa za kujitafutia fedha pasipo kuajiriawa.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!