Home Kitaifa CHUO KIKUU CHA ZANZIBAR (SUZA) KINATOA WATAALAMU WENGI ZAIDI HASA KATIKA FANI...

CHUO KIKUU CHA ZANZIBAR (SUZA) KINATOA WATAALAMU WENGI ZAIDI HASA KATIKA FANI YA KISWAHILI

Na Magreth Mbinga

Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar (SUZA) kimewekeza zaidi katika sekta ya elimu hasa kuwatengeneza vijana kuweza kujiajiri wenyewe wanapo maliza msomo yao waweze kuleta mafanikio kwa jamii na taifa kwa ujumla.

Hayo yamezungumzwa na Makamu Mkuu wa chuo cha (SUZA) Prof .Moh’d Makame Haji wakati wa mahojiano yake na mwandishi wetu katika ufunguzi wa maonesho ya Vyuo vikuu yanayoandaliwa na TCU na kusema kuwa chuo chao kinatoa kozi za afya, biashara, uchumi, fedha, sayansi ya bahari, utalii pamoja na maeneo ya lugha sambamba na elimu kwa ujumla wake.

Pia amesema Mkuu wa chuo hiko ni Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Dk Hussein Ally Mwinyi anahakikisha chuo kinafanya kazi vizuri na kutoa huduma zake katika mazingira bora pamoja na maadili mema.

Tunaangalia sera ya Serikali ya Tanzania na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar kukuza kiswahili ndio maana tunatoa kozi ya kiswahili walio ndani ya nchi ya Tanzania na nje tunatoa katika ngazi ya cheti,astashahada na shahada na shahada ya uzamivu ” amesema Prof Moh’d.

Sanjari na hayo Prof Moh’d amesema huduma zeo zinatolewa katika weledi wa hali ya juu watu wote waliopita SUZA wamepata huduma inayofa na inamuwezesha kufanya kazi zake kwa weledi wa hali ya juu.

Tunakituo maalumu cha kuangalia uboreshaji wa lunga ya kiswahili tumekusanya wataalamu mbalimbali kulingana na mahitaji kutayalisha vitini vya kiswahili ambavyo vitasaidia kukuza kiswahili duniani kote” amesema Prof Moh’d.

Vilevile Prof Moh’d amesema wapo tayali kushirikiana na wadau mbalimbali katika kukuza kiswahili ili kiweze kuenea Duniani kote sababu wao ndio wanatoa wataalamu wengi zaidi na wenye weledi wa hali ya juu hasa katika kozi hiyo ya kiswahili.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!