Home Kitaifa CHUO CHA UTALII(NCT) CHAJA NA MAFUNZO YA MUDA MFUPI URATIBU WA MATUKIO

CHUO CHA UTALII(NCT) CHAJA NA MAFUNZO YA MUDA MFUPI URATIBU WA MATUKIO

Na Magrethy Katengu.

Katika kuhakikisha kunakuwepo na ufanisi wa uratibu na usimamizi wa matukio, Chuo cha Taifa cha Utalii (NCT) kimesema kutakuwa na ushirikiano na Wadau mbalimbali wakiwemo Ma MC waratibu Matamasha, Ili kusaidia Wanafunzi wanaohitimu wawe na weledi wa kutosha kuweza kukidhi soko la Kimataifa la ajira.

Akizungumza wakati wa ufunguzi wa mkutano kati ya Chuo hicho na wadau wa uratibu wa matukio, Kaimu Mkuu wa Chuo hicho, Taaluma, Tafiti, na ushauri Bi. Jesca william amesema lengo la kukutana na wadau hao ni kujadiliana kwa pamoja na kuangalia namna ya kuwajenga uwezo zaidi pamoja na kujua mahitaji halisi ya tasnia hiyo sambamba na kuendelea kutoa mafunzo itakayoendana na mahitaji halisi ya soko la ndani na nje ya nchi..

Amesema NCT inatambua kuwa tasnia hiyo inakuwa kwa haraka na kutoa mchango mkubwa kwa wadau wa tasnia hiyo katika kukuza utalii na kutoa fursa kwa vijana kujiajiri na kuchangia kukuza uchumi wa mtu binafsi na Taifa kwa ujumla.

“Naomba kutoa rai kwa Viajana kujiunga na kozi ya Uratibu wa matukio ambayo inatolewa katika Chuo chetu cha Taifa cha Utalii Kampasi ya Bustani kwani wameona katika nchi za jirani ikiwemo Kenya walio wengi wamesoma yaani kuna utofauti mkubwa kati ya Tanzania na nchi hizo hivyo wabunifu ambao hawajasomea wakipata kozi ya muda mfupi itawasaidia sana kutambulika Kimataifa kutokana na cheti watakachopatiwa” amesema Jesca.

Na kuongeza kuwa “Ni matarajio ya Chuo kuwa wadau mbalimbali watajitokeza kuchangamkia fursa hii ya mafunzo yanayotolewa kwa kushirikiana na Wadau wa tasnia hii ili kuhakiksha washiriki wanapata ujuzi stahiki unaoendana na Soko la sasa la kuratibu na kuendesha shughuli hizi kitalaam zaidi” Ameongeza.

Kwa upande wao baadhi ya washiriki wa mafunzo hayo wakizungumza kwa nyakati MC Mbwanda amemshukuru Chuo huko kimekwenda zaidi hakijajikita tu kwenye fani ya Utalii na ukarimu na kimeanzisha fani hiyo hapo kwani hapo awali haikuwepo watu walikuwa wanajifanyia holela tu pasipokuwa na taaluma walikuwa wanatumia vipaji vyao na ubunifui.

“Watu tulikuwa tunajiendesha wenuyewe kama kuku wa kienyeji hatujawahi kufundishwa popote hivyo imetolewa kurasimishwa hii tasnia yetu hapa nchini imewarahisishia sana kwani hapo awali Ili uweze kujifunza lazima uwende Nairobi kwa kutumia gharama zako hivyo mmetutanilia wigo mpana wa vijana kuzalishwa italeta chachu shughuli zetu kuziendesha Kwa viwango tukiwachukuwa na kuwajiri”amesema MC

Naye Msanii maarufu wa maigizo nchini (Dkt. Cheni) amesema mafunzo hayo yatakwenda kuwaongezea ujuzi ambapo sasa wanakwenda kufanyakazi zao kitaalam.

“Chuo hiki kimekuwa msaada mkubwa kwetu, kwa kuandaa mafunzo haya sasa tunakwenda kufanya shughuli zetu kitaalam zaidi, tunapongeza Uongozi wa Chuo cha Taifa cha utalii kwa kuandaa mafunzo haya” amesema Dkt. Cheni.

Tasnia ya Uratibu wa Matukio ni Sekta inayohusisha watu mbalimbali wakiwemo, Waratibu wa Matukio katika taasisi na watu Binafsi (Events Planners), Waandaaji wa Mikutano mbalimbali (Conference Organizers), Waratibu wa Matamasha mbalimbali, Waratibu wa matukio ya Kitamaduni (Cultural Events), Washereheshaji (MCs), Wapambaji, Wapishi na wadau wengine.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!