Home Kitaifa CHUO CHA USTAWI WA JAMII WAJA NA MWAROBAINI WA UKATILI WA KINGONO...

CHUO CHA USTAWI WA JAMII WAJA NA MWAROBAINI WA UKATILI WA KINGONO KATIKA MITANDAO YA KIJAMII

Chuo cha Ustawi wa jamii kimefanya utafiti kuhusu ukatilia wa kingono hasa kwenye Mitandao ya kijamii ambao unawakumba wanafunzi wa vyuo mbalimbali nchini.

Hayo yamezungumzwa na Prof. Justice Urasa wakati akitolea ufafanuzi mawasilisho ya utafiti ambao utakuwa na manufaa sio kwa wanafunzi tu bali kwa Nchi nzima ya Tanzania.

Pia Prof Urasa amesema utafiti huo umekuja na majibu jinsi gani mwanafunzi atumie mitandao ya kijamii bila kumletea matatizo hayo ya ukatili wa kingono kwani lengo la mwanafunzi ni kupata elimu bila kubugudhiwa na mtu yeyote.

“Tunaendelea kufanya tafiti na kujifunza namna gani tutatokomeza ukatili wa kingono sambamba na watafiti wafanye tafiti za majadiliano wajumuishe madodoso ya mmoja mmoja na makundi ili kupata njia iliyo bora katika taasisi za elimu ya juu “amesema Prof Urasa.

Sanjari na hayo Mkufunzi na Matafiti kutoka taasisi ya Ustawi wa Jamii Itika Gwamaka amesema swala la ukatili wa kingono lipo Duniani kote kwenye tafiti zao zimeonyesha ukatili upo na lazima ukemewe.

“Utafiti utasaidia sana watu watu waone kuwa ukatili upo na jamii au wanafunzi wanapojiunga na taasisi za elimu waelekezwe namna sahihi ya kutumia mitandao ya kijamii ” amesema Gwamaka.

Vilevile Gwamaka amemalizia kwa kusema ukatili upo kwenye maeneo mengi moja kati ya vitu vinavyo fanya wanafunzi wakubwe na janga hilo la ukatili ni maudhui ambayo wanayaona kwenye mitandao ya kijamii yanawezesha kwa asilimia kubwa sana wakutwe na kitendo hiko.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!