Home Kitaifa CHANDI AWATAKA VIONGOZI KUSIKILIZA KERO ZA WANANCHI, AAGIZA ALIYEPORWA ENEO LA “CAR...

CHANDI AWATAKA VIONGOZI KUSIKILIZA KERO ZA WANANCHI, AAGIZA ALIYEPORWA ENEO LA “CAR WASH” KURUDISHIWA

Na Shomari Binda-Musoma

MWENYEKITI wa Chama cha Mapinduzi ( CCM) Patrick Chandi amewataka viongozi wa chama na serikali kusikiliza kero za wananchi na kuzipatia ufumbuzi.

Kauli hiyo ameitoa mjini Musoma ikiwa ni siku ya 3 ya ziara yake ya mkoa mzima kufatilia utekelezaji wa ilani ya uchaguzi ya CCM.

Akiwa kwenye mkutano wa hadhara kwenye viwanja vya Nyasho stend amesema chama hakiwezi kuona wananchi wakilalamika wakati viongozi wa kutatua kero zao wapo.

Amesema muda mfupi wa ziara yake kwenye maeneo aliyopita amewasikiliza wananchi na kubaini wapo viongozi ambao hawatimizi majukumu yao ipasavyo.

Chandi amesema kila mmoja akitimiza majukumu kwenye nafasi yake ikiwa ni pamoja na kuwasikiliza wananchi kero zao hakutakuwa na malalamiko.

“Nashukuru mapokezi mazuri ya hapa Musoma lakini pamoja na yote nitoe wito kwa viongozi kuwasikiliza wananchi na kutatua kero zao”

“Nimeruhusu muda wa maswali mmeona namna wananchi walivyo na kero nyingi ambazo zinafanya waichukie CCM na serikali naomba tutimize wajibu” amesema Chandi.

Aidha Chandi amewapongeza wabunge Vesastus Mathayo wa jimbo la Musoma mjini na Mwita Waitara wa jimbo la Tarime vijijini kwa kutrkeleza ilani kwenye majimbo yao

Kupitia mkutano huo Mwenyekiti huyo wa CCM mkoa wa Mara amemuagiza mkurugenzi wa manispaa ya Musoma kumrudishia eneo la kuoshea magari “Car Wash” mwananchi Nurdin Wandwi ambaye alidai kunyang’anywa na kupewa mtu mwingine.

Aidha maelekezo mengine yaliyotolewa na Mwenyekiti huyo kwa mkurugenzi huyo ni kurudishiwa mikokoteni zaidi ya 50 waliokamatiwa wajasiliamali wa manispaa ya Musoma.

Ziara ya Mwenyekiti huyo itaendelea kesho wilayani Serengeti ambapo anaambatana na wajumbe wa Kamati ya Siasa mkoa wa Mara.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!