Home Kitaifa CHAMA CHA WATUNZA KUMBUKUMBU NA NYARAKA NCHINI WAWASHIKA MKONO WAATHIRIKA WA MAAFA...

CHAMA CHA WATUNZA KUMBUKUMBU NA NYARAKA NCHINI WAWASHIKA MKONO WAATHIRIKA WA MAAFA HANANG’

NA; MWANDISHI WETU – DODOMA

Waziri wa Nchi (Sera, Bunge na Uratibu) Mhe. Jenista Mhagama Amepokea kiasi cha fedha za Kitanzania zaidi ya Shilingi Milioni Tatu (3,000,000) ikiwa ni mchango kwa waathirika wa Maporomoko ya Tope kutoka Mlima Hanang’ kutoka kwa Chama kinachosimamia ustawi wa wafanyakazi wa Serikali na Sekta Binafsi cha Watunza  Kumbukumbu na Nyaraka nchini (TRAMPA)

Akizungumza wakati akipokea kiasi hicho cha fedha kwa Niaba ya Serikali jijini Dodoma leo 21 Disemba 2023, Waziri Mhagama alisema Chama hicho pamoja na kujipambanua katika kusimamia ustawi wa wanachama wake pia kinashiriki katika maendeleo ya Taifa kwa ujumla.

Waziri Mhagama alisema, Binafsi nimefarijika sana kwa chama hiki licha ya kuendesha shughuli zake na harakati za wanachama lakini wameguswa na jambo hili ambalo limegusa Taifa hili.

“Mmejitokeza kuunga Mkono jitihada za Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kutoa mchango wenu kwa waathirika huko Hanang’, na kama tunavyofahamua watunza Kumbukumbu ni watu muhimu sana katika kuendesha shughuli mbali mbali za kuendeleza Taifa letu, na Viongozi wengi wa kitaifa wanaheshimu chama hiki na kutambua mchango mkubwa wa chama hiki.” Alisema

 Tumepata maafa makubwa katika eneo la Katesh na Watanzania wamepoteza Maisha na tukiwa na kundi lingine ambalo linahitaji kusaidiwa ambapo Makazi yameharibika na kupoteza nyumba na Nyumba nyingine kuharibika katika kiwango ambacho hakiwezi kukarabatika, waathirika wanahitaji misaada ya kibinabamu ili Maisha mengine yaweze kuendelea.

“Serikali kwa kiasi kikubwa imeweza kutoa huduma za haraka sana kwa kutumia nguvu na utaalam wa ndani,” alibainisha

Akiongea wakati wa kuwasilisha fedha hizo Mwenyekiti wa Chama cha Watunza Kumbukumbu na Nyaraka Nchini (TRAMPA) Bi, Devotha Mrope, alisema (TRAMPA) kama sehemu ya jamii iliona kuna kuna sababu na haja ya kusaidia  Serikali kwa jambo hilo la dharura ambalo lilitokea, na wanachama waliguswa kwa namna moja na nyingine kuchangia kiasi hicho cha fedha kilichopatikana kwa awamu ya kwanza.

 “Natamani tuendelee na zoezi hili kwa awamu ya pili na kiasi kitakachopatikana tutakiwasilisha kwenye akaunti ya maafa tuliyopewa.” Alisema Bi Devotha.

Aliendela kusema kuwa Chama hicho kinatambua Jitihada kubwa ambayo Serikali imefanya katika suala hili, na kutambua mchango mkubwa wa Serikali katika ustawi wa Chama cha Watunza Kumbukumbu na Nyaraka na Juhudi kubwa ambazo Serikali inafanya katika kuhakikisha Chama hiki kinasonga mbele.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!