Na Magreth Mbinga
Chama cha Waigizaji Tanzania (TDFAA) Mkoa wa Dar es Salaam Julai 30 wanatarajia kufanya utalii wa ndani katika Wilaya ya Kilwa Mkoani Lindi kwa lengo la kutangaza vivutio ambavyo vinapatikana Kilwa kisiwani na songo mnara.
Akizungumza na waandishi wa habari Jijini Dar es Salaam Mwenyekiti wa TDFAA Leonard Piere Mwinuka amesema kama waigizaji na kioo cha jamii wapo sahihi kabisa kumuunga mkono Mh Rais katika kutangaza utalii wa ndani ili kukuza kipato cha Nchi.
“Kazi yetu kama waigizaji ni kuhakikisha yale yote anayoyafanya Mh Rais tunayatangaza kwa ukubwa hasa rukizingatia swala la filamu ya Royal Tour ambayo imeitangaza Nchi yetu na vivutio vyake ambavyo vinapatikana kwa ukubwa zaidi.
Mwinuka amesema wanaenda Kilwa wakiwa na lengi kuu la kuwahimiza Watanzania kutamvua vivutio vya ndani ambapo Kilwa kuna mambo mengi mazuri na makubwa sambamba na kuwataka wananchi kujitokeza kwenye zoezi ka Sensa ili waweze kuhesabiwa kuisaidia Serikali kupata idadi kamili ya watu iweze kutoa huduma za jamii kwa wepesi zaidi.
Aidha Muigizaji wa kike Shamira maarufu kama Bi Staa pia ni Mwenyekiti wa kundi la Sauti ya Mama amesema wamehamasika sana kwenda kufanya utalii Kilwa amesikia ndio mji wa kwanza kujitengenezea noti yake.
“Sisi kama waigizaji tumeungana kwa pamoja kumuunga mkono tunaenda kifua mbele kumwambia Mama asante kwakujua kazi yetu sio ya ubabaishaji kwa sapoti aliyotuonyesha kuwa sanaa ni kazi na sisi pia tunamuonyesha kuwa tuna uhuru wa kufanya kazi yetu “amesema Bi Staa.
Afisa utalii kutoka mamlaka ya usimamizi wa wanyama pori Tanzania (TAWA)Rweja Lugendo wameungana na waigizaji wa Mkoa wa Dar es Salaam kutangaza utalii wa ndani amvao unajenga uchumi ambapo inaongeza kipato cha Nchi .
“Sisi TAWA tupo pamoja nao na Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mh Samia Suluhu Hassan baada ya kutangaza utalii nje na ndani kumekuwa na mwamko mkubwa sana wa wananchi kutembelea vivutio ,watatembelea Kilwa kisiwani na songo mnara”amesema Lugendo.
Rais wa chama cha wataalamu wa figo ambaye pia ni daktari bingwa wa kwanza Nchini Tanzania ambaye anafanya kazi katika Hoapitali ya Taifa ya Muhimbili Dk Onesmo Kisanga amesema nijuhudi muhimu ya kuimarisha utalii wa ndani wao kama wataalamu wa figo wanawaunga mkono waigizaji .
“Wasanii ni watu amvao wapo karibu sana na jamii hivyo itasaidia kuongeza watalii wandani na tutawatumia kutoa elimu ya figo kulingana na utafiti tulioufanya 2014 kaskazini mashariki mwa Tanzania imegunsulika 6.7% ya wananchi wana aumbuliwa na marashi ya figo”amesema Dk Kisanga.