Home Kitaifa CHAMA CHA MAPINZUZI KIMERIDHISHWA NA UONGOZI WA DKT. MWINYI

CHAMA CHA MAPINZUZI KIMERIDHISHWA NA UONGOZI WA DKT. MWINYI

CHAMA Cha Mapindizi (CCM), kimeridhishwa na uongozi wa Rais wa Zanzibar, Dkt. Hussein Mwinyi.

Hayo yamesemwa leo Novemba 4, 2023, na Makamu Mwenyekiti wa CCM, Abdulrahman Kinana, katika maadhimisho ya miaka mitatu ya uongozi wa Dk. Mwinyi.

Kinana amesema Dkt. Mwinyi amejituma sana na kujikita katika kuleta maendeleo ya wananchi wa Unguja na Pemba huku akiwaunganisha kuwa kitu kimoja.

Akiyataja mafanikio yaliyopatikana Zanzibar kwa miaka mitatu tangu Rais Dkt. Mwinyi alipoingia madarakani, Kinana amesema ni pamoja na kuharakisha maendeleo kwa kutekeleza miradi mikubwa ikiwemo ujenzi wa shule, hospitali na miradi ya wananchi ya kiuchumi.

Aidha, amesema amewaunganisha wananchi, hivyo kusahau tofauti za itikadi za kisiasa, na watu wote kuwa wamoja.

Kinana amefafanua kwamba, hatua hiyo inatoa matumaini katika kipindi cha miaka miwili iliyobakia kufikia ukamilikaji wa malengo ya utekelezaji wa ilani ya uchaguzi ya CCM ya 2020-2025.

Rais Mwinyi tunakushuru sana, katika kipindi cha miaka mitatu umefanya mambo makubwa, ikiwemo kuleta mabadiliko makubwa ya maendeleo ya kijamii na kiuchumi, pamoja na kuwaunganisha wananchi na kuimarisha amani na utulivu wa kisiasa,” amesema Kinana.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!