Home Kitaifa CCM YAWASHUKURU WANANCHI NA WANACHAMA WAKE KUWAPA USHIRIKIANO KATIKA ZIARA YAO

CCM YAWASHUKURU WANANCHI NA WANACHAMA WAKE KUWAPA USHIRIKIANO KATIKA ZIARA YAO

Chama cha Mapinduzi CCM kimewashukuru wanachama wake pamoja na wananchi kujitokeza kwa wingi katika ziara yake ya kikazi ya Makamu Mwenyekiti wa CCM bara Abdul Rahman Kinana aliyofanya katika mikoa mitano Simiyu, Manyara, Mara, Tabora , Dodoma katika Wilaya ya Kondoa

Akitoa Shukrani hizo Makamu Mwenyekiti Kinana amesema ameshuhudia namna wanachama na wananchi wanavyoendelea kuchapa kazi na kujihusisha na shughuli za kujiletea maendeleo huku ilani ya Chama cha Mapinduzi (CCM) 2020 – 2025 ikitekelezwa kwa vitendo

Sambamba na hayo Makamu mwenyekiti amewasihi Watanzania kuendelea kuamini uongozi wa nchi unaotokana na Chama cha Mapinduzi kwa kuwa umelenga Maendeleo kama ilivyoahidi wakati wa kampeni za Uchaguzi mwaka 2020

Pia amewapongeza jitihada za serikali katika utekelazaji wa Ilani na kuitaka kuendelea kuwatumikia Watanzania kwa uadilifu na Unyenyekevu kwa kuwa serikali ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania ni zao la watu ..

Aidha Malengo ya Ziara yalikuwa kukagua utekelazaji wa ilani ya Uchaguzi ya CCM ya 2020-2025 uhai wa chama na. kusikiliza. kero za wananchi na kuzipatia ufumbuzi na ziara hiyo waiambatana katibu wa NEC itaikadi na Uenezi Sophia Mjema , Wajumbe wa halmashauri kuu ya CCM Taifa (NEC) Donald Mejiti, Hamoud Jumaa, Munde Tambwe, na Richard Kasesera .

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!