Home Kitaifa CCM YAWAPA MAAGIZO MAWAZIRI WATATU KUTEKELEZA KWA KASI UJENZI WA MIRADI YA...

CCM YAWAPA MAAGIZO MAWAZIRI WATATU KUTEKELEZA KWA KASI UJENZI WA MIRADI YA MAENDELEO KAGERA

Na Theophilida Felician, Kagera

Chama cha mapinduzi CCM kupitia kwa Katibu wa NEC itikadi, uenezi na mafunzo Paul Makonda kimetoa maagizo ya kuwataka mawaziri wa wizara za TAMISEMI, Uchukuzi na Ujenzi kuhakikisha wanafanya jitihada thabiti katika suala zima la utekelezaji wa ujenzi wa miradi mbalimbali ya maendeleo inayotekezwa Mkoani Kagera.

Makonda ameyaagiza hayo hii leo tarehe 9 Oktoba 2023 wakati akiwahutubia wananchi kwenye mkutano wa hadhara mjini Bukoba.

Akiitaja baadhi ya miradi hiyo ni pamoja na ujenzi wa soko kuu Bukoba, kituo cha mabasi Bukoba, ujenzi wa kingo za Mto Kanoni, ujenzi wa barabara ya njia nne Bukoba, barabara za Mkoa Kagera kwa ujumla sambamba na bandari za Kemondo na Bukoba.

Akiwa kwenye mkutano huo Makonda amewasiliana na mawaziri wenye dhamana na wizara hizo moja kwa moja kwa njia ya simu ili kuwaagiza na kuwasisitiza namna chama kinavyowataka kufanya hima nakuhakikisha miradi hiyo inakamilika nakuanza kuwanufaisha wananchi kama ilivyo adhima ya Serikali.

Katika maagizo hayo amemtaka waziri wa TAMISEMI kufika Mkoani Kagera ndani ya kipindi cha muda wa miezi mitatu ili kuishughulikia changamoto ya ujenzi wa soko, kituo cha kisasa cha mabasi ambapo waziri amemjibu kuwa kabla ya kuisha kwa mwezi Desemba mwaka huu 2023 tayari atakuwa ameishafika Kagera kutekeleza maagizo hayo.

Hata hivyo mawaziri wote wameahidi kutekeleza maagizo hayo kwa kasi kama yalivyo matakwa ya Serikali na chama.

Makonda pia amezungumzia malengo makubwa ya CCM chini ya Mwenyekiti wa chama Taifa Mhe Dr Samia Suluhu Hassan katika kuwaletea maendeleo zaidi wana Kagera na wananchi wote hapa nchini.

“CCM ipo kazini muda wote inaendelea kuchapa kazi kwa kasi ni mambo mengi tunayaona kubwa zaidi ni Amani, Amani yetu hii ndiyo inayotuwezesha kufanya haya yote bila amani hakuna litakalofanyika angalieni kwa wenzetu huko hali siyo tulivu kwahiyo wananchi wenzangu tuendelee kuidumisha amani yetu hii” amesema Mhe Makonda.

Katika hatua nyingine kiongozi huyo amesikiliza kero za wananchi nakuzibaini kero kadha wa kadha kutoka kwao hususani kero za migogoro ya ardhi hasa hasa maeneo ya Bukoba mjini ambapo ameuagiza uongozi wa wilaya na Mkoa kufanyia kazi utatuzi wa kero hiyo kwa wananchi ili wapatiwe haki yao.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!