Home Kitaifa CCM YARIDHISHWA UTENDAJI KAZI NA UFATILIAJI MIRADI YA TANROADS MKOA WA MARA

CCM YARIDHISHWA UTENDAJI KAZI NA UFATILIAJI MIRADI YA TANROADS MKOA WA MARA

Na Shomari Binda-Musoma

CHAMA cha Mapinduzi CCM kimedai kuridhishwa na utendaji kazi na ufatiliaji miradi ya barabara inayofanywa na Wakala wa Barabara Tanroads mkoa wa Mara.

Kauli hiyo imetolewa na Katibu wa CCM mkoa wa Mara Ibrahim Mjanakheri alipokuwa akizungumza na Mzawa Blog leo Septembe mosi kwenye mahojiano maalum yaliyofanyika ofisini kwake.

Amesema seeikali ya awamu ya 6 chini ya Dkt.Samia Suruhu Hassan imefanya kazi kubwa kuleta fedha za miradi ya maendeleo na mkoa wa Mara umenufaika.

Katibu huyo amesema eneo la miundombinu ikiwemo ya barabara imepata fedha na Tanrods mkoa wa Mara imefanya kazi nzuri katika kusimamia na miradi inaendelea vizuri.

Amesema katika kipindi cha mvua barabara zote zilikuwa zikipitika na hakuna taarifa yoyote iliyolipotiwa ya barabara kushindwa kupitika kwa kukatika

Mjanakheri amesema hali hiyo ni kuonyesha Tanrods mkoa wa Mara inatekeleza vizuri majukumu yake kupitia usimamizi wa meneja wa mkoa mhandisi Vedastus Maribe na wasaidizi wake.

Amesema ujenzi wa kiwango cha lami barabara ya Makutano Juu-Nyamswa-Ikoma Geti kilometa 135 ujenzi sehemu ya pili ya Sanzate-Natta kilometa 40 wenye thamani ya shilingi bilioni 39,469,855,136.92 unaendelea kusimamiwa vizuri.

Amesema kwenye mradi huo mkandsrasi ameshalipwa na serikali shilingi bilioni 5,048,630,195.46 na kuomba wasimamizi wa masuala ya kibajeti kuiongezea fedha Tanrods mkoa wa Mara ili iweze kukamilisha miradi kwa wakati.

” Kwa mkoa wa Mara ipo miradi mingi ambayo inaendelea na kwa upande wa barabara inatekelezwa vizuri chini ya usimamizi wa Tanrods mkoa wa Mara.

” Kwa dhati tunampongeza meneja wa Tanrods mkoa wa Mara na timu yake kwa kazi wanayoifanya na wanaenda vizuri kikubwa waongezewe kasi ya kupewa fedha ya ukamilishaji”,amesema

Katibu huyo wa CCM mkoa wa Mara ameishukuru serikali ya Dkt.Samia Suluhu Hasaan kwa kutoa fedha nyingi mkoa wa Mara kwaajili ya utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!