Home Kitaifa CCM MWANZA yataka viongozi wasimamie Miradi kwa ukaribu

CCM MWANZA yataka viongozi wasimamie Miradi kwa ukaribu

CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) Mkoani Mwanza kimewataka viongozi wake kuweka juhudi katika kutatua matatizo ya wananchi katika maeneo yao kama inavyosisitizwa na Ilani yake na inayosimamiwa kwa juhudi kubwa na serikali ya awamu ya sita.

Wito huo umetolewa jana wilayani Kwimba na Mwenyekiti wa chama hicho mkoani Mwanza Sixbert Jichab alipokuwa akizungumza na viongozi wa chama, serikali na halmashauri hiyo kuwahimiza kuongeza bidii za kusimamia utendaji kazi ili kuendana na juhudi zinazofanywa kwa sasa katika utekelezaji wa miradi ya maendeleo.

“Mwaka huu jimbo la Sumve wanaletewa sh bilioni 30 katika mradi mmoja tu wa maji sasa huku katika eneo hilo sekta za afya, elimu, miundombinu zikipata fedha nyingi hivyo ni jukumu lenu mfahamu kwa pamoja na kuwaeleza wananchi” alisema Jichab.

Alisema mafanikio yatapatikana pale viongozi wote kwa pamoja wakinuia jambo moja la kuwaletea watanzania maendeleo yao kwani serikali inaleta fedha nyingi za kutekeleza miradi ya maendeleo katika eneo lao.

Jichab aliwataka viongozi kukaa kwa pamoja wakiwa na upendo ili waweze kuwatumikia wananchi waliowachagua kwa mshikamano mkubwa huku wakiwaeleza yale ambayo serikali yao imewafanyia katika maeneo yao.

Mbunge wa Jimbo la Kwimba Shanif Mansoour alisema serikali imeweza kutatua changamoto karibu zote kwenye sekta maji, elimu na afya kwenye eno hilo hata hivyo aliomba juhudi sasa zilekezwe ujenzi wa barabara ya lami kuunganisha na makao makuu ya mkoa.

Aliomba vilevile kusijitokeze tatizo la kuchelewa kufikishwa kwa mbolea ili wakulima waweze kulima kilimo chenye tija kwani watu wengi ni wakulima kwenye eneo hilo.

Mansoor alisema hatua hiyo itawezesha chama hicho kushinda kwa kishindo kutokana na namna ambavyo serikali imeweka juhudi kubwa kutekeleza miradi ya maendeleo.

Naye Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya chama hicho Helen Bugohe aliwataka viongozi hao kuuungana kwa pamoja baada ya uchaguzi kuisha ili waweze kukijenga chama hicho na kupata ushindi kwenye chaguzi zijazo.

Aliwataka wananchama hao kuwa tayari kuhoji kufahamu na kuisimamia vizuri miradi inayotekelzwa kwa faida ya wananchi.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!