Na Neema Kandoro Mwanza
Wanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Mwanza wameadhimisha miaka47 Kwa kupokea wanachama wapya kutoka vyama pinzani lkn pia na kutembea mashina ya Ngazi ya Chama
Wakiongozwa na Mwenyekiti wa Ccm Mkoa wa Mwanza Michael Lushinge Masanja Smart alisema lengo la kushuka kwenye Mashina ni Agizo la Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassani Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Taifa lakini pia alisema Kasi ya Mafakio hayo ni imechochewa na Serikali sikivu Nchini alisema mafanikio yaliyofanyika katika bara Elimu, Masoko, Ustawi wa jamii michezo utamaduni ulinzi na Usalama
Pamoja na hayo Mwenyekiti Smart alisisitiza kuwa Chama chake kimepania kutembelea Viongozi walio Sahihi hivyo hivyo kuwataka wote wanao tarajia kuomba nafasi mbalimbali katika Uchaguzi wa serikali za Mitaa Kujitadhimini
Naye Mjumbe wa Halmashauri Kuu Ccm Taifa NEC Ndg Jamal Babu aliwataka Mabalozi wa Chama hicho kuhakikisha wanahamasisha watu kwenye Mashina Ili wajitokeze kuboresha Taarifa zao kwenye Daftari la Kudumu la wapiga kura na kuhimiza Wanawake kujitokeza na kuwania nafasi mbalimbali
Kwa upande wake Katibu wa CCM Mkoa wa Mwanza Ndugu Omary Mtuwa aliwataka wanachama kuwa wanyenyekevu na kufata maelekezo yote yanayotolewa Kwa Ukubwa Zaidi wa Chama.