Home Kitaifa CCM MUSOMA MJINI YATAKA MIGOGORO YA ARDHI ISHUGHULUKIWE KWA UMUHIMU WAKE

CCM MUSOMA MJINI YATAKA MIGOGORO YA ARDHI ISHUGHULUKIWE KWA UMUHIMU WAKE

MBUNGE MATHAYO KUWASILISHA ALIYOYAFANYA KESHO

Na Shomari Binda – Musoma

WAJUMBE wa Halmashauri Kuu ya Chama cha Mapinduzi (CCM )wilaya ya Musoma mjini wamewaomba viongozi wa chama kufatilia na kushiriki kwenye utatuzi wa migogoro ya ardhi.

Wakizungumza kwenye kikao maalum cha halmashauri kuu kilichofanyika kwenye ukumbi wa CCM mkoa wamesema wananchi wamekuwa wakilalamikia masuala ya ardhi na wanapaswa kusaidiwa kupata utatuzi.

Wamesema viongozi wa chama ngazi ya wilaya kwa nafasi zao washirikiane na wataalam wa ardhi kutatua migogoro ya ardhi.

Katibu wa CCM Kata ya Rwamlimi Paulo Baraka amesema wananchi wanapokuwa wanalalamika wanakigusa chama na kukisema vibaya.

Amesema CCM kama chama tawala inalo jukumu la kuwasaidia wananchi hasa kwenye eneo la migogoro ya ardhi na maeneo mengine.

Katibu huyo amesema iwapo viongozi watashiriki kwenye utatuzi wa migogoro itakijenga chama na kuedelea kushika dola.

Viongozi naomba tushiriki katika suala zima la utatuzi wa migogoro ya ardhi maana imeonekana kuwa kero kwa wananchi.

Tutatue kero za wananchi na hii itatusaidia viongozi na chama katika hali ya kisiasa na tutakuwa pia tumewasaidia wananchi wetu“,amesema Paulo

Mkuu wa wilaya ya Musoma Dk.Khalfan Haule amesema mkoa unaendelea na kliniki ya utatuzi wa migogoro ya ardhi na ulishafanya kikao Musoma mjini na wataendelea na kusikiliza na kutatua kwa itakayojitokeza.

Amesema kama viongozi wa serikali watashirikiana na viongozi wa chama kuhakikisha wanashughulikia migogoro ya ardhi.

Mbunge wa jimbo la Musoma mjini Vedastus Mathayo amesema ipo migogoro inayohusiana wananchi na jeshi la wananchi ambayo amefatilia na kikao baina ya wananchi na jeshi ambacho kitafanyika hivi karibuni kupata uamuzi.

Mbunge Mathayo amesema kwenye kikao cha Mkutano Mkuu Maalum disemba 20 ataelezea masuala mbalimbali ya utekelezaji wa ilani katika jimbo la Musoma mjini katika masuala mbalimbali ikiwemo miradi ya maendeleo.

Aidha wajumbe hao wamezungumzia hali ya kisiasa wilaya ya Musoma mjini ndani ya Musoma mjini ni nzuri na kutakiwa kila mmoja kushiriki katika kukijenga na kukiimarisha chama.

Katika masuala hayo ya kukijenga chama Mwenyekiti wa kikao hicho ambaye ni Katibu wa CCM wilaya ya Musoma mjini Burhan Ruta amesema lipo jukumu la kuongeza wanachama na jukumu hilo ni la kila mmoja.

Kuelekea uchaguzi wa serikali za mitaa mwakani Mwenyekiti huyo amesema maandalizi yanapaswa kuendelea ikiwa ni pamoja na kuwaandaa kisaikolojia watakaojitokeza kuomba nafasi hizo.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!