Home Kitaifa CCM MUSOMA MJINI YAMPONGEZA RAIS DKT.SAMIA UTOAJI FIDIA BILIONI 3.9 KWA WANANCHI

CCM MUSOMA MJINI YAMPONGEZA RAIS DKT.SAMIA UTOAJI FIDIA BILIONI 3.9 KWA WANANCHI

Na Shomari Binda-Musoma

CHAMA cha Mapinduzi( CCM) Wilaya ya Musoma mjini kimempongeza na kumshukuru Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan kwa kutoa fedha kiasi cha biliini 3.9 kwa wananchi wa Musoma.

Kiasi hicho cha fedha kimetolewa kwa wananchi wa Kata ya Nyasho na Kamnyonge kwaajili ya kupisha upanuzi wa uwanja wa ndege wa Musoma.

Katibu wa CCM Wilaya ya Musoma mjini Burhani Ruta amesema fedha hizo zitawasaidia wananchi kwenda kupata makazi mengine na kupisha upanuzi wa uwanja.

Amesema serikali ya Rais Dkt.Samia ni sikivu na lilikuwa suala la muda na tayari fedha hizo zimefika kwaajili ya wananchi hao.

Katibu Burhani amesema wananchi watakaopata fidia hiyo ya kupisha eneo la upanuzi wa uwanja wakatumie fedha hizo kwa malengo mazuri ikiwa ni kupata makazi mapya.

Amesema si vyema kuingiza fedha hizo kwenye matumizi yasiyofaa na baadae kuziacha familia zikiangaika.

” CCM Wilaya ya Musoma mjini tunamshukuru Rais Dkt.Samia kwa kutoa fidia ya bilioni 3.9 kwa wananchi wa Nyasho na Kamnyonge.

” Wananchi wakatumie fedha hizo vizuri ikiwa ni pamoja na kwenda kuanzisha makazi mapya maeneo mengine ili kuendeleza maisha”,amesema.

Katibu huyo amesema kupisha kwa wananchi eneo la upanuzi wa uwanja wa ndege Musoma kutapeleka kuendelezwa kwa ujenzi wake.

Amesema kukamilika kwa ujenzi huo kutainua uchumi wa Musoma mjini ikiwemo shughuli za utalii watakaopitia hapo kuelekea hifadhi ya Serengeti na maeneo mengine.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!