Home Kitaifa CCM MKOA WA MARA YASEMA HAITAKUWA KIKWAZO KWA MBUNGE MATHAYO KUTEKELEZA MAJUKUMU...

CCM MKOA WA MARA YASEMA HAITAKUWA KIKWAZO KWA MBUNGE MATHAYO KUTEKELEZA MAJUKUMU YAKE

Na Shomari Binda-Musoma

CHAMA cha Mapinduzi (CCM) kimesema hakitakuwa kikwazo kwa mbunge wa jimbo la Musoma mjini Vedastus Mathayo kutekeleza majukumu yake ikiwemo utekelezaji wa ilani.

Kauli hiyo imetolewa na Katibu wa CCM mkoa wa Mara Ibrahim Mjanakheri wakati wa fainali ya mashindano ya Mathayo Cup 2023.

Amesema ilani ya uchaguzi ya CCM ya 2020 had 2025 inazungumzia pia michezo na kwa jimbo la Musoma mjini inatekelezws kwa asilimia 100.

Katibu huyo amesema amepata uhamisho wa kuamia mkoa wa Mara hivi karibuni lakini ameshuhudia namna mbunge huyo anavyofanya kazi ya kupongezwa.

“Nimefatilia mashindano haya nimeona namna yanavyovutia watu wengi na utekelezaji wa ilani na CCM inakupongeza sana mheshimiwa Mathayo”

.“Chama cha Mapinduzi hakitakuwa kikwazo kwako bali endelea kuchapa kazi na tunakuunga mkono kwa hiki unachokifanya” ,amesema.
Mjanakheri

Kwa upande wake mbunge wa jimbo la Musoma mjini Vedastus Mathayo amesema ataendelea kuandaa mashindano mbalimbali ili kuinua vipaji vya vijana na kuwaweka pamoja.

Amesema baada ya mashindano haya kumalizika mwezi novemba yataanza mashindano mengine kwa timu za umma na taasisi.

Katika fainali hiyo iliyochezwa kwenye uwanja wa Mara sekondari na kuhudhuriwa na mashabiki rukuki ilishuhudiwa timu ya Mwigobero ikiibuka na ushindi na kuwa mabingwa kwa mikwaju ya penati 15-14 dhidi ya Nyamatare fc baada ya piga nikupige.

Kwa kuchukua ubingwa huo Mwigobero wamepata zawadi ya ng’ombe na kombe,mshindi wa pili laki 4 na mbuzi mmoja,mshindi wa tatu amepata laki 2 na mbuzi mmoja pamoja na zawadi mbalimbali.

Wakati huo huo jeshi la polisi mkoani Mara limemshukuru mbunge Mathayo kwa kyandaa mashindano hayo na kuyatumia kutoa elimu juu ya kuzuia uhalifu na wahalifu.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!