Home Kitaifa CCM MARA YAWAPIGA TAFU WAUGUZI HOSPITAL YA MKOA

CCM MARA YAWAPIGA TAFU WAUGUZI HOSPITAL YA MKOA

Na Shomari Binda-Musoma

CHAMA cha Mapinduzi (CCM) mkoa wa Mara kimechangia kiasi cha shilingi milioni 6 kuwezesha mradi wa duka la dawa la chama cha wauguzi (TANNA) tawi la hospital ya rufaa ya mkoa wa Mara.

Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Mara Patrick Chandi ametoa kiasi cha shilingi milioni 4 huku mjumbe wa baraza kuu la UWT taifa, Rhobi Samwelly,akichangia kiasi cha shilingi milioni 2.

Akizungumza kwenye maadhimisho ya siku ya wauguzi duniani kwa mkoa wa Mara kwa niaba ya Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Mara, mjumbe wa baraza kuu la UWT taifa, Robby Samwelly, amesema wauguzi wanafanya kazi kubwa hivyo wanahitaji kusaidiwa.

Amesema wauguzi huduma yao inaokoa maisha ya binadamu kwa kutoa huduma za kiutu hivyo changamoto zao jamii inapaswa kuzitatua pale inapopatikana nafasi.

Rhobby amesema wauguzi wanapaswa kupewa ushirikiano na kila mmoja na sio kusubili pale wanapokuwa wanatoa huduma wakati wakitekeleza majukumu yao.

Nipo hapa kumwakilisha Mwenyekiti wa CCM mkoa na nimwsikia wauguzi mna mradi wenu wa duka la dawa Mwenyekiti amewachangia milioni 4 na mimi namuunga kwa milioni 2.

Hii itaongeza mtaji wenu na itawasaidia kutatua changamoto ikiwemo kulipia leseni za wauguzi ili muendelee kutimiza majukumu yenu”,amesema Robby.

Kaimu mganga mfawidhi wa hospital ya rufaa ya mkoa wa Mara,Elias Saganya, amesema upo upungufu wa wauguzi ambao wanapaswa kuongezwa kwenye hospital hiyo.

Amesema mchango uliotolewa na viongozi hao wa CCM ni msaada mkubwa kwa mradi wa wauguzi ws duka la dawa na utawasaidia.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!