Na Magrethy Katengu
Katibu Nec, Itikadi na Uenezi Taifa Chama cha Mapinduzi CCM Komredi Paul Makonda amesema Chama katika kuanzia mwaka 2023,2024 kila robo ya mwaka watahakikisha wanakaa na viongozi wote kutathimini kazi zilizofanyika ikiwemo utatuzi wa migogoro, Utekelezwaji wa miradi mbalimbali ili kusaidia Nchi inakwenda kwa kasi kubwa kiuchumi.
Ameyasema hayo leo Jijini Dar es salaam katika Mkutano wa Waandishi wa habari ambapo amesema katika maendeleo yote lazima kuwe na mkakati madhubuti wa kusikiliza wananchi wanasema nini kwani sasa Viongozi wote kuanzia ngazi ya kata kijiji, Wialaya na Mkoa waache tabia ya kukaa na kusubiria mpaka ziara za viongozi wakubwa wapite bali wawe na utaratibu wa kukaa vikao na wananchi wao kusikiliza kero zao.
“Chama kinatoa rai kwa wale wote ambao wanashauku ya kutaka Ubunge, Udiwani kuanza kupita na kufanya mikutano ya kampeni kwani muda bado hivyo nawasihi waacheni waliopo wafanye kazi hadi hapo kampeni zitakaporuhisiwa rasmi kuanza kwani Uongozi ni Kudra za Mwenyezi Mungu” Amesema Paul Makonda
Hata hivyo akizungumzia Ziara yake ya kikazi aliyoifanya hivi karibuni katika Mikoa mbalimbali ikiwemo Dodoma alikutana na Uhaba wa maji baadhi ya vijiji na Migogoro ya Ardhi hivyo akaagiza Waziri wanaohusika kushughulikia kero hizo mara moja
Sanjari na hayo akitoa mrejesho wa Ziara katika Kanda ya Ziwa amesema Shi Bilion 14 zilitolewa na Rais Kuunganisha barabara katika kiwango cha lami Mkoani Mwanza Km 2.294 na Tsh Bilioni 6 kutumika kwa Mradi wa maji Katoro Geita
Hata hivyo amesema zaidi ya Mikoa 25 imefikiwa na Waziri wa Ardhi kwa utatuzi wa Migogoro ya Ardhi, Matokea chanya yaonekana.
“Idara ya Uenezi tulifanya ziara, tulitoa maelekezo ikiwemo kutokana na kero za migogoro ya ardhi na maji na tulielekeza wizara kutatua kero hizo, na Wizara ya Ardhi ilianzisha utamaduni wa kuwa na kliniki za Ardhi na Waziri Jerry alianzia mkoani Dodoma ambapo zaidi ya Wananchi elfu 41 wamepewa hati, Waziri ameshatembelea mikao 25 kutatua migogoro ya ardhi maana yake kazi inafanyika katika kufanya kazi kumuondolea machungu na maumivu mtanzania pasipo kujali chama chake.”
“Lakini CCM imemuagiza Waziri wa Ardhi kuhakikisha tunapata mwarobaini wa migogoro ya ardhi ili kero hizi kuisha kabisa na sasa wameanza kutekeleza agiza hili na wanataka kufanya mpango wa sera za ardhi, tayari wamesimamishwa kazi wafanyakazi 15 waliobainika kuzalisha migogoro na Wizara inajipanga kutumia vema mifumo wa Tehama, CCM inatoa pongezi katika hili“
“Mkoani Kagera, Waziri wa Tamisemi Mhe. Mchengerwa tayari amesaini mkataba wa miradi 15 ikiwemo mkoa wa kagera kuhusiana na utatuzi wa Stendi na Masoko”
“Mkoani Geit zaidi Tsh Bilion 6 zishatolewa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, kwa ujenzi wa mradi wa maji Katoro na Geita wenye uwezo wa kubeba kaya zaidi ya elfu 68000 na mradi umefikia zaidi ya asilimia 98% na hadi kufikia mwishoni mwa mwezi huu Disemba basi Maji safi na salama yatapatikana kwa wingi na kwa uhakika.”
Aidha, Mwenezi Makonda amebainisha kuwa tayari Waziri wa Ujenzi Mhe. Bashungwa ameshashuhudia utiaji saini wa mkataba wa ujenzj wa Daraja la Sukuma lenye urefu wa Mita 70 na barabara unganishi yenye urefu wa Kilomita 2.294 kwa kiwango cha lami.
Katika kikao hiko Paul Makonda akijibu maswali yaliyoulizwa na Waandishi wa habari amesema Serikali imejenga Masoko ili kuboresha mazingira ya Wafanyabiashara licha ya changamoto ya Masoko hayo wafanyabiashara kukihama kwa kukosa wateja ameahidi kuwa watajitahidi wanatembelea hayo masoko yanayolalamikiwa kuwa hayana wafanyabishara kutatua kero zinazosababisha .
Aidha CCM inawatakia kila na Kheri Wananchi wote kuelekea sikukuu za kumaliza Mwaka 2023 hivyo sikukuu hizo wazisherekee kwa kufuata sheria na kwani katika kipindi hiko kunatokea ajali na kusababisha vifo,walemavu hivyo Jeshi la Polisi siku hizo wahakikishe wanafanya operesheni kila mahali ili kupunguza ajali zisizo za lazima.