Home Kitaifa CCM KATAVI WAMPONGEZA RAIS KURUHUSU MIKUTANO YA HADHARA.

CCM KATAVI WAMPONGEZA RAIS KURUHUSU MIKUTANO YA HADHARA.

Chama cha Mapinduzi CCM mkoa wa Katavi leo Januari 05 2023 kimefanya kongamano la kumpongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan kwa kuondoa zuio la mikutano ya hadhara.
Kongamano hilo limefanyika katika ukumbi wa mikutano wa Mpanda Social Hall mjini Mpanda lilitanguliwa na maandamano yaliyobeba ujumbe wa pongezi kwa Rais wa Tanzania kwa hatua yake ya kuruhusu Demokrasia kwa vyama vyote vya siasa nchini kufanya mikutano ya hadhara.

Akizungumza katika kongamano hilo mwenyekiti wa CCM mkoa wa Katavi Idd Kimanta amesema hatua hiyo ni busara ya mwenyekiti wa Chama hicho Taifa kuruhusu mikutano ya siasa kufanyika bila zuio.
Kimanta amewataka viongozi na wanachama wa chama hicho mkoani humo kujiandaa kujibu hoja ikitokea zimeibuliwa na vyama vya upinzani kwa njia ya amani na kuendelea kusema mema yaliyofanywa na serikali ya awamu ya sita.


Kwa upande wake mkuu wa mkoa wa Katavi Mwanamvua Mrindoko ametoa rai kwa vyama vya siasa kutumia fursa hiyo kunadi sera zao na kufanya siasa za kiungwana badala ya kutoa lugha za kejeli majukwaaani.
Amesema kwa upande wa serikali mkoa utasimamia mazingira sawa kwa kila chama kuendesha shughuli zake za kisiasa ikiwemo mikutano ya hadhara kwa kuweka ulinzi na usalama bila kubagua.
Shughuli za mikutano ya hadhara ya siasa nchini zilizuiliwa tangu mwaka 2016 baada ya aliyekuwa Rais wa awamu ya tano Hayati John Magufuli kushika hatamu za uongozi.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!