Home Kitaifa CAG APATA UKAKASI MIRADI UJENZI WA MASOKO YA SAMAKI , MAENEO YA...

CAG APATA UKAKASI MIRADI UJENZI WA MASOKO YA SAMAKI , MAENEO YA BIASHARA TANGA JIJI

NA BONIFACE GIDEON,TANGA

MKAGUZI na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) Mkoa wa Tanga amebaini uwepo wa dosari namna ya uendeshaji wa miradi ya masoko ya samaki huku miradi hiyo ikishindwa kutoa faida licha ya kuonekana Serikali kuwekeza fedha nyingi kupitia sekta hiyo ya Uvuvi.

Aidha Halmashauri hiyo imeonekana kupunguza kiwango cha hoja zilizoibuliwa na CAG kwa Mwaka wa fedha 2021/2022 kutoka hoja 44 hadi kufikia hoja 41 huku hoja nyingi zikionekana kujirudia kila mwaka hali iliyoonekana kuwakasirisha viongozi wengi wa Halmashauri hiyo hususani Madiwani na Mkuu wa Mkoa huo Waziri Kindamba.

Hoja hizo za CAG ziliibuliwa jana juni 19 wakati wa kikao cha Baraza la Madiwani kilichoketi kwamujibu wa Sheria kujadili Ripoti ya Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG),

Kikao hicho kiliongozwa na Mwenyekiti wake ambaye pia ni Mkuu wa Mkoa wa Tanga Waziri Kindamba na kuchambua hoja 41 ambazo CAG amezitolea kwenye Ripoti yake ya mwaka wa fedha 2021/2022 na zinatakiwa zifanyiwe kazi kabla ya mwaka wa fedha kufungwa juni 30 mwaka huu.

Katika hoja zake CAG ameonesha kutokuridhishwa na namna Halmashauri hiyo inavyoendesha na kusimamia Masoko ya Samaki huku Mapato yatokanayo na Sekta ya Uvuvi yakionekana kupotea kutokana na isimamizi mbovu, Masoko hayo ni Mchukuuni,Tongoni na Deepsea huku soko kuu la Samaki Kisosora likinyooshewa vidole na Madiwani kufanyiwa ukarabati na ili kudhibiti upotevu wa mapato.

Katika Ripoti yake , CAG amesema kutokufurahishwa na mazingira mabovu ya kufanyia Biashara katika soko la Deepsea huku kwakiwango kikubwa masoko mengine kutokufanya kazi kwa ufanisi.

Akijibu hoja hiyo ya masoko ya Samaki , Mkurugenzi wa Jiji la Tanga Spora Liana alisema

‘’Tumetenga mil.300 kwaajili ya ukarabati na ujenzi wa vizimba vya kuuzia Samaki soko la Deepsea, kuhusu Masoko mengine ya Tongoni na Mchukuuni yapo kwenye mradi wa Botnar foundation lakini pia wavuvi tuliwanunulia Boti kwaajili ya kuwahamasisha kuanza kufanya kazi ya uvuvi’’ alisisitiza Liana

Hoja hiyo imeonekana kumkasirisisha Mkuu wa Mkoa Tanga Waziri Kindamba na kutoa tamko hili

‘’Tanga jiji ndio kioo cha Mkoa wa Tanga na Mikoa ya Kanda ya Kaskazini Mashariki,sisi tuna ukanda mzuri wa Bahari na ndio mgodi wetu wa Madini tunaoutegemea kwenye vitu vingi ikiwamo kitoweo cha Samaki aina mbalimbali ambao hawapatikani huko katika mikoa ya Bara,Mkurugenzi hakikisha unawapeleka Wataalamu wako hata huko Pemba waende wakajifunze uchumi wa Buluu ili tuende sawa kwapamoja, tunahitaji uchumi wetu ukue hasa kupitia Bahari yetu ambayo wengine wanaililia ‘’ alisema Waziri Kindamba

Miradi mingine ambayo CAG ameitilia shaka ni Kuchelewa ujenzi wa jengo la Stendi mabasi kange, mfumo mbovu wa ukusanyaji mapato eneo mapumziko forodhani ,Fremu za maduka ya Biashara za Stendi ya Pongwe ambayo inafremu za maduka 88 lakini mfumo wa mapato hauonyeshi kulipiwa ambapo hadi sasa kwa Mujibu wa Ofisa Biashara wa Halmashauri hiyo Lusia Malando ni Sh 400,000 kati ya mil.3 pekee ndizo zimelipiwa kinyume na makubaliano kati ya Wanyabiashara na Halmashauri kutokana na kuwa Fremu hizo hazikujengwa na Halmashauri bali Wafanyabiashara kwamakubaliano maalumu.

Mwisho

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!