Home Kitaifa BULAYA AGUSWA NA TATIZO LA FEDHA ZA WASTAAFU NA UHAMISHO ZA ASKARI...

BULAYA AGUSWA NA TATIZO LA FEDHA ZA WASTAAFU NA UHAMISHO ZA ASKARI POLISI

Na Shomari Binda-Musoma

MBUNGE wa viti maalum mkoa wa Mara, Ester Bulaya amesema kuna tatizo la wastaafu na uhamisho kwa askari wa jeshi la polisi hapa nchini.

Akiuliza swali la nyongeza kwenye Wizara ya Mambo ya Ndani bungeni hii leo, Bulaya amesema kumekuwa na tatizo kubwa kwa askari wakiwemo wa Mkoa wa Mara hasa kwenye malipo ya wastaafu na uhamisho.

Amesema askari wanaokuwa wanapewa uhamisho kutoka eneo moja kwenda jingine wamekuwa hawapewi kwa wakati fedha za kubebea mizigo.

“Nashukuru mheshimiwa Naibu Spika kwa kunipa nafasi ya kuliza swali la nyongeza,tatizo la wastafu ni kubwa pamoja na wastafu wakiwemo wa mkoa wa Mara je, Wizara imejipangaje kumaliza tatizo hilo” aliuliza.

Ajijibu swali la mbunge huyo, Waziri wa Mambo ya Ndani, Yusuf Masauni,amesema serikali ina dhamira njema kwa wastafu wa jeshi la polisi.

Amesema bajeti kwa kila mwaka imekuwa ikitengwa kuweza kufanya malipo ya askari polisi wanaomaliza utumishi wao.

Waziri huyo amesema kazi ya uhakiki kwa wastaafu umekuwa ukiendelea ili kuandaa malipo ya wastaafu hao wa jeshi la polisi.

“Uhakiki wa mapema wa madeni ya wastaafu umekuwa ukiendelea kwa wachache waliobaki ili kuwahisha ulipaji” ,amesema.

Akiendelea kujibu maswali ya wabunge walioulizia kwenye Wizara hiyo, Waziri Masauni amesema Wizara imeendelea kuthamini kazi inayofanywa na askari wa jeshi la polisi na masrahi yao na mazingira ya kazi na makazi yataendelea kuwekwa vizuri.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!