Home Afya BUKOBA DC YA PAMBANA KUHAKIKISHA JAMII INATUMIA UNGA WA VIRUTUBISHI ILI KUBORESHA...

BUKOBA DC YA PAMBANA KUHAKIKISHA JAMII INATUMIA UNGA WA VIRUTUBISHI ILI KUBORESHA LISHE

Theophilida Felician Kagera.

Imeelezwa kwamba katika hali ya kupambana na changamoto ya kuutokomeza utapiamlo na udumavu Halmashauri ya Bukoba Mkoani Kagera jitihada mbalimbali zimekuwa zikifanyika ili jamii iweze kutumia vya kula vilivyorutubishwa ikiwemo unga uliongezewa virutubishi.

Ameyasema hayo Afisa lishe wa Halmashauri hiyo Janeth Mahona wakati akiwasilisha taarifa ya utekelezaji wa afua zalishe kwenye kikao kazi kilichonyika kata Kemondo.

Janeti amefafanua kuwa suala la kuhamasisha jamii juu ya kutumia unga maalumu uliongezewa virutubishi kwa sasa limevaliwa njuga kwani tayari unga huo umeishaanza kuzalishwa maeneo kadhaa ya Halmashauri ya Bukoba.

Amesema tayari zipo mashine 7 za mfano ambazo zinaendelea kusindika unga wa namna hiyo ambapo kata Kemondo zipo mashine 6 na moja ipo kata Katoro hivyo unga huo uliongezewa virutubishi unatumiwa kwa baadhi ya wananchi japo siyo kwakiwango kikubwa , nguvu imeelekezwa shuleni ili watoto wote waweze kutumia uji wa unga huo wa lishe na tayari zipo shule chache zinazotumia unga huo.

Ameeleza licha ya shule chache 25 kutumia unga huo wa lishe bado shule zinaendelea kutoa chakula shuleni ambapo zipo shule 199 za msingi na sekondari, shule 155 ni za msingi, na 44 ni za sekondari shule zinazotoa chakula kwa zaidi ya mlo mmoja kwa shule za msingi ni 16 nashule 139 zinatoa mlo mmoja ambao ni uji na shule 13 kati ya shule 44 za sekondari zinatoa chakula zaidi ya mlo mmoja huku 31 zikitoa mlo mmoja ambao ni uji.

Amesema uhamasishaji unaendelea kwa kasi kwa wadau ili wajitokeze na kuzalisha unga huo maeneo mengi ya Bukoba kuliko ilivyo kwa sasa hiyo ikiwa nisambamba na kuwaelimisha wananchi umuhimu wa kutumia vya kula hivyo vilivyorutubishwa ukiwemo unga huo na watu wameanza kubadilika na kutumia vyakula hivyo.

Amewahakikishia wadau kwamba unga huo unaozalishwa na watu binafsi unakuwa salama kwani maafisa afya ngazi ya kata na wilaya wamekuwa wakishughulikia hilo kwa
ukaribu.

Hata hivyo ameongeza kwamba Halmashauri ya Bukoba imejizatiti zaidi katika kutekeleza mkataba wa lishe kama yalivyo maelekezo ya Serikali.

Kikao hicho kikihudhuriwa na wadau kutoka kada tofauti tofauti wakiwemo maafisa lishe PANITA ambao ni jukwaa la lishe Tanzania linalotekeleza miradi wa urutubishaji chakula shuleni wameyaeleza mambo kadha wa kadha juu ya kuzingatia suala lishe kwa jamii.

Lubango Charles ni Afisa lishe wa mradi huo katika utangulizi amesema kuwa ili kuweza kuupunguza udumavu ni lazima kuhimiza matumizi sahihi ya vya kula vilivyorutubishwa na vyakula mchanganyiko vya makundi matano ambayo ni matunda, mboga mbonga, wanyama, samaki na vinginevyo.

Ameeleza adhima ya mradi huo ni pamoja na kujenga imani juu ya matumizi ya chakula kilichorutubishwa katika jamii na shuleni ambapo ulianza mwaka wa 2021 hivyo uhamasishaji kwa jamii unahitajika zaidi ili wananchi wote wawe na ufahamu wa matumizi ya vyakula hivyo na umuhimu wake.

Febronia Boniface naye akiwa Afisa lishe kutoka PANITA amewasilisha mada kwa upana juu ya maana ya lishe bora na lishe duni.

“Lishe duni imekuwa ikiyasababisha madhara kwa jamii hususani ya utapiamlo na udumavu hivyo wakati ni sasa wa kuwajibika na kuyatokomeza matatizo haya, kitaifa kiwango cha udumavu kimepungua kutoka 34% kwa mwaka 2014 na kushuka kwa 31% kwa mwaka 2018 hivyo bado hali ni mbaya kwani kwa mjibu wa vigezo vya shirika la afya duniani WHO kiwango kinachokubalika kitaifa ni 20% sasa tuko 31% mikoa inayoongoza kwa viwango vya juu sana vya udumavu ni Iringa, Njombe, Rukwa, Ruvuma, Geita na Kagera ikiwa ya sita kwa 34.3% ukiangalia hii mikoa yote ni mikoa ambayo inaongoza kwa uzalishaji wa chakula Tanzania lakini ni mikoa ambayo inaongoza kwa udumavu ni wapi tunakosea? nini kifanyike? ndo maana tuko hapa” ameeleza Afisa Febronia.

Amebainisha kuwa tatizo kubwa linaloathiri jamii ni upungufu wa madini joto, vitamini na virutubishi na waathirika wengi ni watoto chini ya umri wa miaka mitano na wanawake waliokatika umri wa kuzaa hivyo yapaswa watu kula vyakula vya makundi hayo ili kubolesha afya.

Wadau kutoka makundi mbalimbali akiwemo Afisa lishe Mkoa Jaoanitha Jovin, wahudumu wa afya ngazi ya jamii, viongozi wa dini, siasa, wasindikaji wa unga, nawengineo kwa pamoja wamechangia namna ya kuongeza nguvu katika kutekeleza habari ya lishe kwakuifikia jamii nakuhamasisha jinsi ya kula vyakula vyenye mlo kamili ili kunusuru matatizo ya udumavu na utapiamlo.

Hata hivyo wito umetolewa kwa ngazi zote kuanzia afya, walimu, wanasiasa na makundi mengine wawajibike ipasavyo kuifikia jamii kwa vitendo na hali hiyo ikizingatiwa itasaidia kupunguza udumavu hivyo diwadi wakata ya Kemondo Musaa Kayoza amewahidi wadau kuwa kwakushirikiana na watendaji wengine ndani ya kata atahakikisha kata yake inakuwa ya mfano katika utekelezaji wa shughuli hizo za lishe.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!