Mkurugenzi Idara ya Menejimenti ya Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge na Uratibu Brigedia Jenerali Hosea Ndagala amefanya ziara ya kutembelea Wilaya ya Kigamboni kata ya Mjimwema Mtaa wa Maweni kwa lengo la kuangalia athari zilizotokea kutokana na Mvua zinazoendelea kunyesha Jijini Dar es Salaam.
Amefika kwaajili ya kupata taarifa kuhusu hali halisi ya athari ya mvua hizo kwa Wilaya ya Kigamboni alielezwa kuwa maeneo yaliyoathirika ni pamoja na Mtaa wa Maweni eneo la Bondeni kata ya Mji Mwema pamoja na Maweni eneo la Biasi ambayo yamezingirwa na maji ya mvua zinazoendelea kunyesha Katika Mkoa huo.
Aidha Serikali kupitia Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge na Uratibu itaendelea kuratibu masuala ya menejimenti ya maafa nchini ili kuhakikisha jamii inaendelea kuwa salama na stahimilivu dhidi ya maafa.
Walianza safari katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam na kufika katika kikao cha pamoja na Katibu Tawala Msaidizi (Mipango na Uratibu) Chillah Moses.