Home Kitaifa BRELA YAWAJENGEA UWEZO MAOFISA BIASHARA KANDA YA KASKAZINI

BRELA YAWAJENGEA UWEZO MAOFISA BIASHARA KANDA YA KASKAZINI

Maofisa Biashara wametakiwa kuwa na tabia ya kuwatembelea Wafanyabiashara katika maeneo yao ili kuweza kuibua na kujua changamoto zao badala ya kuwatembelea wakati wa kuwadai Kodi na leseni.
Hayo aliyasema mkuu wa Wilaya Tanga Hashim Mgandilwa Wakati akifunga Mafunzo ya Siku Tano ya Kuwajengea Uwezo Maofisa Biashara kutoka Mikoa ya Arusha,Kilimanjaro,Manyara na Tanga yaliyofanyika katika ukumbi wa mkuu wa Mkuu wa Mkoa wa Tanga.


Aidha Aliwataka Maofisa Biashara hao kuwa Karibu na Wafanyabiashara na Wananchi ili kutoa huduma Bora,saidizi na elimishi kwa Wafanyabiashara na kuongeza kipato Chao na Serikali kupata Kodi,

Kwa tafiti ndogo iliyofanyika kuhusu utendaji wa maofisa Biashara imebainika kuwa kumekuwa na uelewa hafifu wa Sheria ya leseni za Biashara sura ya 208 na Maofisa Biashara Wengi kutumika kama wakusanya mapato hasa Sehemu za Biashara ,vilabuni nna kwenye Nyumba za kulala wageni badala ya kuwa Wasaidizi na washauri kwa Wafanyabiashara na wawekezaji.” Alisema Mgandilwa.

Sambamba na hayo aliwataka kutoa huduma saidizi kwa Wananchi kwa weledi na uaminifu mkubwa huku wakijiepusha kabisa na vishawishi vya kuomaba na kupokea rushwa katika utoaji wa huduma hizo ili Mafunzo hayo yaoneshe matokeo chanya kama ilivyokusudiwa na Serikali.

Akizungumzia lengo la kufanya Mafunzo hayo kwa maofisa Biashara Mkurugenzi wa leseni kutoka BLERA Andrew Mkapa Alisema kuwa lengo la Mafunzo hayo ni kuhakikisha huduma zinazotolewa na Maofisa zinawafikia wananchi kwa Karibu zaidi hivyo kuwapunguzia kero za usumbufu na gharama zisizokuwa za lazima katika urasimishaji wa Biashara hapa Nchini.

Alisema kuwa BRELA pamoja na wakala na Mamlaka ya Serikali za miataa inafanya kazi kwa kuzingatia Sheria moja hivyo hawajawahi kukutana na pamoja hivyo kupitia Mafunzo hayo Sasa wanamekutana kubadilishana uzoefu jambo ambalo litasaidia wao kufanya kazi kwa weledi huku wakizingatia Sheria.


Aliongeza kuwa kupitia Mafunzo hayo maofisa Biashara wapatao 80 Kupitia Mikoa ya Kanda ya Kaskazini na Halmashauri zao wamepatiwa Mafunzo ili Kuwajengea Uwezo wa utendaji kazi kwa uelewa mkubwa .
Linda Mabele Afisa Biashara kutoka Ofisi ya Rais Tami semi Dodoma Alisema kuwa Mafunzo hayo yatakuwa na tija pale ambapo maofisa watafuata Sheria na utaratibu na kuhahakisha wanakuwa Mahusiano Mazuri Wananchi Wafanyabiashara .

Aliongeza kuwa kufuata Sheria Kuna faida nyingi ikiwamo kuwarahisishia kutekeleza wajibu wao kwa Ufanisi zaidi ili kuimarisha uchumi wa watanzania kwa kutenda haki.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!