Na Shomari Binda-Musoma
MAAFISA biashara 138 kutoka mikoa 10 hapa nchini wametakiwa kuwa marafiki wa wafanyabiashara na sio maadui katika kuinua uchumi wa taifa.
Licha ya kutokuwa maadui wametakiwa pia kutumia mafunzo waliyoyapata kutoka Brela kuwa chachu ya kuwainua wafanyabiashara na kuwa walipa kodi wazuri.
Kauli hiyo imetolewa na Katibu Tawala wa mkoa wa Mara Robert Makungu wakati akifunga mafunzo ya siku 3 ya maafisa biashara hao yaliyotolewa na Wakala wa Usajili wa Leseni na Biashara (Brela).
Amesema yapo makubaliano ya kuondoa vikwazo kwa wafanyabiashara hivyo maafisa biashara wanalo jukumu la kuwasaidia wafanyabiashara.
Makungu amesema Brela imetimiza jukumu lake na sasa maafisa biashara waliopata mafunzo wakatimize majukumu yao.
Akizungumzia mkoa wa Mara,Makungu amesema yspi maeneo mengi ya uwekezaji na kuwakaribisha wawekezaji kwaajili ya uwekezaji.
“Niwashukuru sana Brela kwa kuleta mafunzo haya mkoa wa Mara kwani ni sehemu salama na haina shida””Niwashukuru sana Brela kwa kuleta mafunzo haya mkoa wa Mara kwani ni sehemu salama na haina shida”
Wakati mwingine mkipata nafasi mje mkoa wa Mara kwa shughuli nyingine za Brela” ,amesema Makungu.
Baadhi ya washiriki wa mafunzo hayo wamesema watakwenda kufanyia kazi mafunzo hayo na kuwa mabalozi wazuri.
Wamesema wanakwenda kufanya kazi kwa ushirikisno wa karibu na wafanyabiashara ili malengo yaliyokusudiwa yaweze kutimia.