Home Kitaifa BRELA YATOA ELIMU YA MILIKI UBUNIFU , WIKI YA ELIMU, UJUZI NA...

BRELA YATOA ELIMU YA MILIKI UBUNIFU , WIKI YA ELIMU, UJUZI NA UBUNIFU.

Afisa Msaidizi Usajiri Mwandamizi kutoka kurugenzi ya Miliki Ubunifu ya BRELA, Nassoro Mtavu akizungumza na wadau mbalimbali wakati wa maadhimisho ya wiki ya Elimu Ujuzi na Ubunifu jijini Tanga

Na Boniface Gideon -TANGA

Wakala wa Biashara na Leseni ‘BRELA’, wameendesha zoezi la kutoa Elimu ya alama Miliki Ubunifu Bunifu kwa Wateja na Wadau mbalimbali wanaotembelea banda la ‘BRELA’ ,kwenye maonyesho ya Wiki ya Elimu, Ujuzi na Ubunifu yanayofanyika katika Viwanja vya Popatilal Jijini Tanga.

Akitoa Elimu kwa Wadau na Wamiliki wa Biashara, Msaidizi wa Usajili Mwandamizi kutoka kurugenzi ya Miliki Ubunifu,Nassoro Mtavu amesema ni vyema kila mtu akapata Elimu ya Mlipakodi ili aweze kusajili Biashara na Leseni ,

Kazi kubwa ya maonyesho haya ni kutoa Elimu ya ufumbuzi na alama za Biashara na huduma,kwetu sisi tumeichukulia hii kama fursa ya kutoa Elimu,na tukumbuke kuwa sehemu ya Elimu hii ni uvumbuzi,na sisi Brela uvumbuzi ndio kazi kubwa tunayoifanya ,wengi hawafahamu nini Cha kufanya baada ya kuvumbua kitu , kwahiyo tunachokifanya nikuwapatia Elimu sahihi nini chakufanya baada ya kuvumbua” Amesisitiza Nassoro

Amesema wataendelea kutoa Elimu juu ya Usajili wa Biashara na Leseni nakuwataka wadau mbalimbali kuhakikisha wanasajili huduma mbalimbali wanazozitoa,

tunawaomba Wadau wetu wasajili huduma wanazozitoa ili ziwe na vibali ,na sisi tupo tayari wakati wowote kutoa huduma,na tutaendelea kushirikiana na Wadau wetu na wasichoke kutuuliza pale wanaposhindwa kutimiza vigezo“Amesema Nassoro

Amesema kwasasa kusajili Biashara na kupata Leseni za ‘BRELA’ ni rahisi na wanaweza kupata huduma kwanjia ya mtandao,

Unaweza kupata huduma kwanjia ya mtandao, pia tunawaomba wavumbuzi waje kwetu ,waache kusikiliza maneno ya mtaani mana watapotoshwa na watapata Elimu isiyo sahihi” Amesema Nassoro

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!