Na Magrethy Katengu
Wakala wa Usajili leseni za biashara Brela imesema wmwitikio wa watu kusajili kampuni na biashara zao katika maonyesho viwanda yaliyoandaliwa na Shirikisho la Viwanda CTI na Mamlaka ya Biashara Tantrade yaliyofanyika Ukumbi wa Diamond Jublee na kutembelea Banda lao na kuomba ushauri ulikuwa wa kuridhisha.
Akizungumza Jijini Dar es salaam Afisa usajili lesseni Brela Ndeyanka Mbowe wakati wa kufungwa. maonyesho ya hayo amesema maonyesho hayo yanafanyika kwa mara ya kwanza hivyo amewasihi wale ambao hawajasajili bKampuni zao au logo za bidhaa zao kufika ofisini kuendelea na usajili kwani ni ni Koda kisheria kuuza bidhaa ikiwa na jina bila usajili.
“Maonyesho haya yamekuwa yakipekee sana na tumekutana na wadau wetu wamilili wa viwanda vya nje na za ndani walookuja kushiriki na baadhi ya wafanyabiashara wamekuja kutembelea ukumbi huo nao wakiwa kuona teknolojia na bidhaa zinazozalishwa’ amesema Mbowe
Tanzania Manufacture Expo ni maonyesho ya kwanza kufanyika hivyo tunaomba CTI na Tantrade wasiishie hapo mwakani tena yawepo. kwa kipekee. zaidi.
Aidha Maonyesho hayo yalifungwa na Mkuu wa Mkoa Mhe Albart Chalamila kwa kutembelea mabanda na kujionea Teknoloji mbalimbali.