Home Kitaifa BRELA NA TIRDO WAKUTANA KUJADILI MFUMO WA TAKWIMU ZA VIWANDA

BRELA NA TIRDO WAKUTANA KUJADILI MFUMO WA TAKWIMU ZA VIWANDA

Menejimenti ya Wakala Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA), imekutana na Wataalamu kutoka Shirika la Utafiti wa Maendeleo ya Viwanda (TIRDO), kujadili kuhusu uanzishwaji wa mfumo wa takwimu za viwanda.

Majadiliano hayo yamefanyika leo tarehe 5 Oktoba, 2023 katika ofisi za BRELA jijini Dar es Salaam.
Akizungumza katika kikao hicho, Mkurugenzi Mkuu wa TIRDO Prof. Mkumbukwa Mtambo amesema, lengo la mfumo huo ni kuwa na kituo kimoja cha kupata takwimu za viwanda tofauti na ilivyo sasa.

“Hivi sasa takwimu za viwanda zinapatikana katika taasisi tofauti tofauti, mathalani taarifa za kiwanda kidogo zinapatikana SIDO, viwanda vikubwa zinapatikana BRELA na kutoka taasisi nyingine, hivyo uanzishwaji wa mfumo wa viwanda utawezesha kuwa kituo kimoja cha kupata taarifa za viwanda,” amesema Prof. Mtambo.

Akitoa maelezo kuhusu mfumo huo, Afisa TEHAMA wa TIRDO, Bi.Elizabeth Mtegwa, amesema katika utekelezaji wa zoezi hilo TIRDO imeanza kupita mikoa mbalimbali nchini kukusanya takwimu za viwanda, kwa kuanzia imekwishapata takwimu za viwanda katika mikoa ya Pwani, Morogoro na Dar es Salaam.

Kwa upande wake Afisa Mtendaji Mkuu wa BRELA, Bw. Godfrey Nyaisa amesema, BRELA iko tayari kushirikiana na TIRDO katika kuhakikisha kuwa, mfumo wa taarifa za viwanda unakamilika mapema iwezekanavyo.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!