Home Kitaifa Brand ya bidhaa za Zanzibar (Made in Zanzibar) kuhuishwa upya Zanzibar –...

Brand ya bidhaa za Zanzibar (Made in Zanzibar) kuhuishwa upya Zanzibar – Soraga

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais – Kazi, Uchumi na Uwekezaji Mhe. Mudrik Ramadhan Soraga amebainisha kuhuishwa upya kwa brand ya bidhaa za Zanzibar.

Ameyasema hayo wakati akijibu swali la Mwakilishi wa Jimbo la Mwanakwerekwe Mhe. Ameir Abdallah Ameir katika mkutano wa Kumi mkutano wa Kumi kikao cha tatu cha Baraza la Wawakilishi kinachoendelea huko Chukwani Nje kidogo ya Mji wa Zanzibar.

Amesema kupitia Sera ya Taifa ya Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi Zanzibar ya mwaka 2022, imezingatia uhamasishaji wa matumizi ya bidhaa za ndani pamoja na kuihuisha ‘Brand’ ya bidhaa za Zanzibar (Made in Zanzibar) sambamba na kuhamasisha wananchi kuzithamini bidhaa zao za ndani.

hatuna budi kuwa na mashirikiano ya wadau wote ili kuhamasisha matumizi ya bidhaa za ndani kupitia majukwaa mbali mabali na sehemu nyingine wanazozifikia tunaandaa vipindi maalaum katika vyombo vyetu vya habari kwa ajili ya kutangaza na kuhamasisha utumiaji wa bidhaa za ndani.” Alisema Soraga

Pia Waziri Soraga amesema Wakala wa Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi Zanzibar inawasaidia na kuwashajiisha Wajasiriamali katika masuala ya kuimarisha ubora wa bidhaa ili ziweze kupata Hati za ubora wa viwango nchini ili bidhaa zetu ziweze kuwa na ushindani ulio sawa na bidhaa za nje.

Sambamba na hayo ameeleza kuwa suala la kuimarisha masoko kwa bidhaa za Wajasiriamali ni kipaumbele kikubwa cha Serikali na mikakati inaendelea kufanyiwa kazi kupitia Ofisi ya Rais Kazi, Uchumi na Uwekezaji ipo katika hatua ya kutafuta ufumbuzi wa suala la upatikanaji wa vifungashio hapa nchini ili kuimarisha ubora wa bidhaa za Wajasiriamali.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!