Na Boniface Gideon -ARUSHA
Kampuni ya Utalii kupitia huduma za kulala ya Bougainvillea group of lodges imewaomba wa Watanzania kufanya Utalii wa ndani,
Mkurugenzi wa kampuni hiyo Nico Ombay amewaambia Waandishi wa Habari leo kwenye maonyesho ya Utalii Mkoa wa Arusha maarufu kama ‘KILIFAIR‘,kuwa kwasasa Utalii wa ndani ni gharama nafuu zaidi,
“nawaomba Watanzania tuupende Utalii wetu,tunavyo vivutio vingi sana ambavyo vitakufanya mtu ufurahie maisha,tuna ngorongoro na Serengeti na vivutio vingine vikubwa ambavyo vinavutia zaidi, kufanya Utalii kuna faida nyingi sana ikiwemo kuondoa msongo wa mawazo na kuimarisha Mahusiano na familia yako“Amesema Ombay
Ombay amesema kampuni yao imejipanga kufanya upanuzi zaidi wa uwekezaji na kuongeza uwanda mkubwa zaidi wa ajira kwa Vijana,
“tunaendelea kuongeza uwekezaji wetu kwenye vivutio vingine vikubwa zaidi ukiacha Ngorongoro na Serengeti,tutaongeza zaidi katika maeneo mbalimbali Nchini, lakini pia kubwa zaidi ni ajira kwa Vijana zitaongezeka zaidi” Amesisitiza Ombay
Amewataka Vijana kusomea masuala ya Sekta ya Utalii kutokana na kuwa na uwanda mpana zaidi wa fursa za ajira,
“Sekta ya Utalii inanafasi nyingi sana za ajira kwa Vijana waliosomea mambo ya Utalii,hivyo niwaombe Vijana ambao hivi sasa wanasoma,basi wasiache kusomea masuala ya Utalii lakini pia kwa Wazazi wasiache kuwasomesha Watoto wao hasa wakihitaji kusomea masuala ya Utalii“Amesema Ombay