Home Michezo BONANZA LA MICHEZO LANOGESHA SIKU YA MZUMBE NA KAMBI YA UJASIRIAMALI

BONANZA LA MICHEZO LANOGESHA SIKU YA MZUMBE NA KAMBI YA UJASIRIAMALI

Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Mzumbe, Prof. William Mwegoha amesema Chuo hicho kitaendelea kudumisha utamaduni wa michezo baina ya wafanyakazi na wanafunzi ili kudumisha umoja, mshikamano na kukuza vipaji mbalimbali.

Amesema hayo tarehe 20.3. 2024 katika bonanza la michezo lilofanyika Chuo Kikuu Mzumbe Kampasi Kuu, Morogoro ikiwa ni katika ufunguzi wa siku ya kwanza ya Siku ya Mzumbe na Kambi ya Ujasiriamali 2024 “Mzumbe Day and Entrepreneurship Camp”  

Nawapongeza wote, niseme tumeburudika vya kutosha, siku imekuwa nzuri ya bonanza, nia na dhamira yetu ni kuunga umoja kati ya wafanyakazi na vijana wetu, “Staff – Student bonanza”, mambo yote yanayohusu changamoto za michezo tunayafanyia kazi, ubora wa viwanja, vifaa vya michezo na jezi za michezo” amesisitza Prof. Mwegoha.

Prof. Mwegoha amewapongeza timu ya wanafunzi kwa kuibuka kidedea kwa goli 4-3 dhidi ya timu ya wafanyakazi. Michezo mingine iliyochezwa ni pamoja na mpira wa wavu na kikapu. Kwa upande wa Kaimu Naibu Makamu Mkuu wa Chuo Taaluma, Tafiti na Ushari Prof. Eliza Mwakasangura na Naibu Makamu Mkuu wa Chuo mipango, Fedha na Utawala, Prof. Allen Rangia Mushi  wamezipongeza timu hizo kwa kushiriki kikamilifu katika bonanza hilo.

Awali akizungumza Kaimu Meneja wa Ubunifu, Ujasiriamali na Uhusiano wa Kitasnia Chuo Kikuu mzumbe, Dkt. Emmanuel Chao ameushukuru uongozi wa Chuo  kwa kutenga siku ya wajasiliamali kwa lengo kukuza vipaji na bunifu za wanafunzi na wafanyakazi, jambo ambalo linaongeza ufanisi wa chuo katika kutatua changamoto za jamii.

Siku ya Mzumbe na Kambi ya Ujasiriamali inafanyika kwa siku tatu kuanzia tarehe 20 – 22 Machi 2024 Chuo Kikuu Mzumbe Kampasi Kuu Morogoro ikiongozwa na  kaulimbiu “Kuzingatia Teknolojia Zinazoibukia na Njia Mpya za Kujifunza kwa Ajili ya Ukuaji Endelevu”

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!