Home Kitaifa BODI YA WAKURUGENZI AKIBA COMMERCIAL BANK YAMTANGAZA MWENYEKITI WAKE MPYA

BODI YA WAKURUGENZI AKIBA COMMERCIAL BANK YAMTANGAZA MWENYEKITI WAKE MPYA

Bodi ya Wakurugenzi ya Akiba Commercial Bank Pic (ACB) inapenda kutangaza uteuzi wa Mwenyekiti wake mpya, Bi. Catherine N. Kimaryo. Bi Kimaryo ni kiongozi mahiri, mwenye weledi na mbobezi katika nyanja za ukuaji na ufanisi wa biashara kutokana na uzoefu wake katika utoaji wa masuluhisho, mbinu, mielekeo ya kimkakati na dira za kibiashara zinazolenga kuleta mabadiliko yenye matokeo chanya. Bi. Kimaryo ndiye mwanzilishi na Mtendaji Mkuu wa NCL, kampuni ya ushauri inayolenga kuimarisha uongozi na u fa nisi wa kimkakati wa watu binafsi na mashirika.

Bi. Kimaryo anachukua nafasi hiyo kufuatia kustaafu kwa Bw. Ernest S. Massawe ambaye aliwahi kuwa Mwenyekiti wa Bodi kwa miaka kumi iliyopita ambapo aliweza kutoa mchango mkubwa katika ukuaji na maendeleo ya Benki ya ACB kwa ujumla. Chini ya uongozi wake thabiti, Bodi na Menejimenti ilifanikiwa kukabiliana na nyakati zenye changamoto ikiwa ni pamoja na janga la kimataifa la UVIKO-19.

Mwenyekiti wa Bodi (Bi. Kimaryo) analeta hazina kubwa ya maarifa kufuatia uzoefu wa miaka zaidi ya 20 katika sekta ya fed ha hususan taasisi za kibenki na uwekezaji kwenye nchi na masoko yanayoibukia barani Afrika na katika bara nyingine kadhaa.

uongozi na utawala. Mbali na Bodi ya ACB, Bi. Kimaryo anahudumu kama Mkurugenzi katika bodi nyinginezo ndani na njeya nchi. Kwa ujumla, Bodi ya Wakurugenzi na Menejimenti ya ACB inampongeza Bi. Kimaryo na inategemea kutumia hazina kubwa ya maarifa, utalaamu, uzoefu, ari na weledi wa Mwenyekiti wao mpya kutimiza maono na mkakati wa Benki unaongozwa na agenda kuu ya mabadiliko. Bi. Kimaryo ana Diploma ya Juu ya Utawala (INSEAD, Ufaransa); Shahada ya Uzamili ya Utawala wa Biashara (Wits Business School, Afrika Kusini); na Shahada ya Kwanza ya Biashara (Chuo Kikuu cha McGill, Canada).

Aidha, Bi. Kimaryo pia ni mzungumzaji wa umma aliyebobea, mshauri, msimamizi na mwendeshaji mijadala mbali mbali hasa katika tasnia ya fedha.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!