Home Kitaifa BODABODA HESHIMUNI SHERIA ZA BARABARANI KUEPUKANA NA AJALI

BODABODA HESHIMUNI SHERIA ZA BARABARANI KUEPUKANA NA AJALI

Na Magrethy Katengu

Mkuu wa Dawati la Elimu ya Usalama Tanzania TRAFIC ACP Michael Delali amewataka wanaosafirisha abiria kwa chombo cha pikipiki kutii sheria ya zizowekwa ikiwemo ya uvaaji kofia ngumu wa na abiria pia kuacha tabia ya kubeba abirua zaidi ya mmoja (Mishkaki) ili kusaidia kupunguza vifo vitokanavyo na ajali za pikipiki .

Agizo hilo amelitoa Jijini Dar es salaam wakati akizindua Kampeni ” vaa kofia achana na mshiko ” mafunzo ya bodaboda yatakayotolewa na taasisi isiyo ya kiserikali Tunaweza Forum itakayoendeshwa 2023/2024 ndani ya miezi 10 katika wilaya ya Kinondoni, Temeke, Ubungo , Ilala, na Kigamboni lengo kwa kushirikina na Wadau mbalimbali ikiwemo NSSF, UTT AMIS , NMB, ORXY na Jeshi la. polisi.

Hata hivyo amesema taasisi hiyo wameweza kushirikiana na wadau mbalimbali ili kusaidia kutoa elimu kwa watumia vyombo vya moto maarufu kama bodaboda ili kusaidia kupunguza tatizo la kutovaa kofia ngumu abiri wakati anatumia chombo cha moto hata ajali ikitokea kupona ni bahati nasibu .

“Sheria ya usalama barabarani iko kwa ajili ya kunusuru ajali lakini imekuwa ikivunjwa utakuta kuna mtindo bodaboda hajavaa kofia abiria hajavaa kofia mwendo mkali alafu dereva mwenyewe pia kavaa ndala ikitokea breki ikifeli Kisigino cha mguu ndiyo kitageuzwa. breki na barabara zetu kokoto lazima ajali itokee hivyo abiria kabla ya kupanda pikipiki mkagua dereva wako na akuvalishe kofia ngumu “ amesema ACP

Kwa upande wake Mwenyekiti wa taasisi. isiyo ya kiserikali Tunaweza. Forum Zabron Kamoga amesema katika kampeni yao watakwenda na fursa mbalimbali kwa bodaboda ikiwemo wataalamu kuwafundisha kuweka. akiba kwa maisha ya baadae, kufungu akaunt. ya NMB kuomba mikopo, kuwekeza kwa UTT AMIS NSSF

Naye Saidy Mpota ameshukuru taasisi hiyo kwa kuweza kuwatambua bodaboda na kuwaletea fursa za kuwekeza fedha zao kwa ajili ya uzeeni au pale wanapopata majanga na wanapenda wandelee na moyo huo kam Rais Dkt Samia Suluhu Hassani alivyowapenda na kuwaletea mikopo katika halmashauri wanakopa kwa vikundi vyao na wanajikwamua kiuchumi huku wakirejesha kidogokidogo bila riba yeyote.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!