Na.WAF, Dodoma
Waziri wa Afya Ummy Mwalimu leo amezindua kitabu cha Mwongozo wa wa utoaji Dawa (Benjamin Mkapa Hospital Formulary) utakaotumiwa na waandika Dawa (Prescribes), Wafamasia,Wachunguzi na Wauguzi katika hospitali ya Benjamin Mkapa jijini Dodoma.
Kitabu hicho kimekuja ikiwa ni kutekeleza wa agizo lake la kuhakikisha dawa zinapatikana ndani ya Hospitali na kuondoa usumbufu wa wagonjwa kwenda kutafuta dawa nje ya hospitali.
Mwongozo huu umeandaliwa kwa kuzingatia Mwongozo wa Matibabu Tanzania na Orodha ya Taifa ya Dawa Muhimu (Standard Treatment Guideline of Tanzania and National Essential Medicine List) ambao unalenga kukuza matumizi sahihi ya dawa kwa wagonjwa wanaopatiwa matibabu Hospitalini hapo ili kuboresha afya zao.
Pia, Mwongozo huu utasaidia katika kuongeza upatikanaji wa dawa kwenye hospitali kwa kuwa unaainisha orodha ya dawa zinazohitajika zaidi hapo hospitalini na kuondoa wigo mpana wenye dawa nyingi ambazo huwa ni vigumu kupatikana hapa nchini.
Utekelezaji wa mwongozo huu utapunguza gharama zisizo za lazima kwenye ununuzi wa dawa na vifaa tiba.