Home Burudani BINGWA MSIMU WA PILI TV3 BILA CHENGA

BINGWA MSIMU WA PILI TV3 BILA CHENGA

SHINDANO la Bingwa Msimu wa pili latambulishwa Watu maarufu mitandao ya kijamii wajitosa , Washiriki 20 kuingia kambini Julai 30,2023 Jijini Dar es Salaam.

Akizungumza na Wanahabari Leo Julai 18,2023 Jijini Dar es salaam, Meneja Mradi wa shindano hilo Ombeni Phiri amesema bingwa ni zaidi ya burudani ambapo msimu wa kwanza waliingia washiriki 18 ambao wengi wao ni vijana wenye ushawishi mkubwa kwenye mitandao ya kijamii na mmoja wao aliibuka mshindi na gari aina ya crown pamoja na pesa taslim.

Hata hivyo ameeleza lengo la kuwepo kwa shindano hilo ni kuwapa fursa vijana Kujifunza vitu mbalimbali ikiwemo fursa zilizopo katika mitandao ya kijamii katika kukuza na kutengeneza brand zao.

Aidha kwa upande wake Meneja Masoko wa Kampuni ya Startimes David Malisa ameeleza kuwa kupitia Msimu wa kwanza walipokea maoni mbalimbali kutoka kwa watazamaji namna ambavyo wangependa msimu ujao uboreshwe kwa baadhi ya vitu na ndio sababu iliyopelekea mwaka 2022 kusiwepo kwa shindano hilo.

Pia amesema Shindano hilo ni daraja la kufunguka kwa fursa nyingi kwani Hata usipofanikiwa kushinda unaweza kupata fursa ya kuwa balozi wa Makampuni.

Harmorapa alikua miongoni mwa washiriki kwa msimu uliopita hivyo kampuni ya Startimes iliweza kumpa ubalozi wa mwaka mmoja ambapo fursa ya ushiriki wake ilianzia hapo kuonekana hakutoka mtupu pamojana washiriki wengine walipata viinua mgongo vyao.

Pia Malisa amewaambia watazamaji wa bingwa kulipia visimbuzi vyao kwani msimu wa pili una maudhui tofauti tofauti yenye kufunza ambapo hata watazamaji watapata elimu mbalimbali.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!