Home Kitaifa BILIONI 776.6 ZAELEKEZWA KATIKA UJENZI, UKARABATI NA MATENGENEZO YA BARABARA VIJIJINI NA...

BILIONI 776.6 ZAELEKEZWA KATIKA UJENZI, UKARABATI NA MATENGENEZO YA BARABARA VIJIJINI NA MIJINI

OR-TAMISEMI

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Mhe. Innocent Bashungwa amesema katika mwaka wa fedha 2022/23 ujenzi wa barabara kwanKiwango cha lami utakua na urefu wa km 422, Kiwango cha changarawe urefu wa km 11,074, Madaraja 269 na Matengenezo kwa barabara yatakayofanyika ni ya urefu wa km 21,595.

Ameyasema hayo Agosti 14, 2022 katika hafla ya utiaji saini mikataba kati ya TARURA na Mandarasi watakaotengeneza kazi za ujenzi, ukarabati na matengenezo ya miundombinu ya barabara kwa mwaka wa fedha 2022/23 ambayo mgeni rasmi alikuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan.

Bashungwa amesema bajeti ya ujenzi, ukarabati na matengenezo ya barabara vijijini na mijini imeongezeka kutoka Shilingi bilioni 272.56 mwaka 2020/21 hadi Shilingi bilioni 722 katika mwaka wa fedha 2021/22 sawa na ongezeko la asilimia 185.

Mwaka wa fedha 2022/23 ni mwaka wa pili wa utekelezaji wa Mpango Mkakati ambapo TARURA imetengewa bajeti ya jumla ya Shilingi bilioni 838.16 ambapo kati ya hizo Shilingi bilioni 776.63 ni fedha za ndani na Shilingi bilioni 61.53 ni fedha za nje.

Amesema Ofisi ya Rais-TAMISEMI ilitoa maelekezo kwa TARURA kuanza taratibu za manunuzi mapema ili kazi ziweze kuanza kabla ya kipindi cha mvua ambapo tayali TARURA ilitangaza zabuni 1,085 zenye thamani ya Shilingi bilioni 378.56, sawa na asilimia 60% ya fedha zilizopangwa kutekeleza miradi ya barabara za vijijini na mijini, kwa mwaka wa fedha wa 2022/2023.

Bashungwa amesema mpaka sasa miradi iliyotayari kusainiwa ni mikataba 968, yenye thamani ya Shilingi bilioni 248.74, na miradi yenye thamani ya Shilingi bilioni 129.83, imetangazwa upya baada ya Wakandarasi walioomba kutokidhi vigezo.

Aidha, Amesema kupitia Mradi Agriconnect kwa ufadhili wa Jumuiya ya Ulaya (EU), barabara zenye urefu wa kilomita 65 kwa kiwango cha lami zitajengwa kwa gharama ya Shilingi bilioni 37.6.

Pia, Amsema katika mwaka 2021/22, Serikali iliweza kuajiri wahandisi 255, ambao kati ya hao wahandisi 185 walielekezwa katika Mamlaka za Serikali za Mitaa, ambapo unapeleka fedha nyingi kwa ajili ya ujenzi wa miundombinu mbalimbali ya halmashauri, Wahandisi 56 walielekezwa katika Sekretarieti za Mikoa, ambazo zina jukumu la ufuatiliaji wa miradi ya maendeleo, na wahandisi 14 walielekezwa TARURA.

Vile vile, Ameeleza katika mwaka wa fedha 2021/2022 yaliagiza magari 130 kwa ajili ya usimamizi wa miradi ya barabara, na tayari yameshapokelewa magari 4, na wanaendelea kufuatilia upatikanaji wa magari 126 ambayo hayajapokelewa.

Wakati huo huo, ametoa wito kwa Makandarasi pale wanapofanya kazi katika maeneo mbalimbali katika halmashauri kutimiza jukumu lao la kulipa kodi husika (Service Levy) na wanapoandaa zabuni zao wakumbuke sehemu ya kodi ambazo huchangia kwenye mapato ya halmashauri zinazopaswa kulipwa.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!