Home Kitaifa BILIONI 3 ZA RAIS SAMIA KUTUMIWA NA TARURA KUFUNGUA BARABARA NA UJENZI...

BILIONI 3 ZA RAIS SAMIA KUTUMIWA NA TARURA KUFUNGUA BARABARA NA UJENZI WA MADARAJA JIMBO LA MUSOMA MJINI

Na Shomari Binda-Musoma

ZAIDI ya shilingi bilioni 3 zinatarajiwa kujenga barabara kilometa 96, madaraja 8 na kalavati 30 ndani ya jimbo la Musoma mjini.

Fedha hizo zinatokana kupitia mfuko wa barabara,mfuko wa jimbo na fedha za tozo ambazo kwa pamoja zimetengwa kukamilisha miradi hiyo.

Hayo yamesemwa na meneja wa Tarura wilaya ya Musoma mhandisi Joseph Mkwizu mara baada ya kumpitisha mbunge wa jimbo la Musoma mjini Vedastus Mathayo kuona miradi ya barabara itakayotekelezwa kwa mwaka wa fedha 2023/2024.

Mkwizu amesema fedha hizo zitalenga matengenezo ya kawaida, sehemu korofi, matengenezo ya muda maalumu, ujenzi wa makalavati na madaraja.

Amesema Kata zote za pembezoni zitafikiwa kwenye barabara zake kwaajili ya kuzifungua pamoja na ujenzi wa madaraja na kalavati.

Mheshimiwa mbunge tumepokea fedha zaidi ya bilioni 3 kutoka serikalini na tupo tayari kuzitumia kwa kazi kusudiwa kwa uhadilifu mkubwa ikiwa ni kufungua barabara na ujenzi wa madaraja na kalavati” amesema Mkwizu.

Kwa upande wake mbunge wa jimbo la Musoma mjini, Vedastus Mathayo,ameendelea kuishukuru Serikali ya awamu ya 6 chini ya Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan,kwa kutoa fedha nyingi jimbo la Musoma mjini.

Mathayo amesema ndani ya jimbo hasa katika maeneo ya pembezoni kazi kubwa imefanyika katika bajeti iliyopita eneo la miundombinu ya barabara na katika bajeti ya 2024/2024 zimetengwa fedha tena kwa kazi zaidi.

Wananchi ambao wamekutana na mbunge huyo akifatilia utekelezaji wa ilani kwenye Kata zao wamemshukuru kwa ufatiliaji wake na kupelekea barabara kufunguliwa na kupitika.

Katika eneo la Bweri wananchi hao wameshukuru kusikia hivi karibuni utaanza ujenzi wa daraja kuunganisha kati ya Nyabisare na Nyamitwebili ambapo kipindi cha mvua wamekuwa wakipata shida kuvuka.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!